WAZAZI WATAKIWA KUWA WASIMAMIZI WA KWANZA KATIKA MALEZI YA WATOTO


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Nchini limewataka wazazi kuwa wasimamizi wa kwanza katika malezi ya vijana wao kipindi wapo nyumbani hata kipindi wanachorejea mashuleni.

Hayo yamesema leo decemba 07 2023 na msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP DAVID MISIME ambapo amewa amewaomba wazazi kushirikiana na Jeshi hilo kuwalinda watoto 

Ameongeza kuwa madereva madereva wa vyombo vya moto wazingatie utamaduni unaosisitizwa na Jeshi hilo wa kufuata sheria na kanuni za usalama Barabarani na kujiepusha na matendo yatayohatarisha usalama wa watoto wanaorudi mashuleni 

SACP MISIME amewaonya baadhi ya madereva kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuwaumiza watoto kimwili na kisaikolojia.

0/Post a Comment/Comments