ASKARI JWTZ APANDISHWA KIZIMBANI


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam, 24 Februari 2023

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ), MT 89487 CPL Hamis Ramadhan (36) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka ya kukataa amri halali.

Mshitakiwa huyo amesomewa shitaka jana na wakili wa serikali Vailet Kyendesya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,  Rahim Mushi.

Kyendesya alidai mnamo  Februari 7,  Mwaka huu mshitakiwa akiwa eneo la Mlimani City barabara ya Survey, Kinondoni, Dar es Salaam akiendesha gari namba T. 433 ALB Nissan Patrol alisimamishwa eneo la kivuko cha watembea kwa miguu na Askari Polisi ambapo alikaidi na kuanza kumsukuma Askari kwa gari yake.

Kyendesya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshitakiwa alikana makosa yake na kuachiwa Kwa dhamana.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Machi 6, mwaka huu kwaajili ya kutajwa. 

0/Post a Comment/Comments