NCC KUENDELEA KUTOA MIONGOZO KUBORESHA SEKTA YA UJENZI

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi –NCC akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akieleza kuhusu yanayofanywa na serikali kwa Maendeleo ya Taifa kupitia sekta ya ujenzi na Taasisi hiyo.

........................

Baraza la Taifa la Ujenzi -NCC limesema litaendelea kuhakikisha miongozo na kanuni zinaanzishwa,zinachapishwa na zinawezesha sekta ya ujenzi kuwa na utekelezaji unaojali taaluma na misingi ya tija Ili miradi inayotekelezwa iwe inafikia Thamani halisi ya Fedha inayotekeleza miradi hiyo.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Baraza Hilo Dkt Matiko Samsoni Mturi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu yanayofanywa na serikali kwa Maendeleo ya Taifa kupitia sekta ya ujenzi na Taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa ili kuhakikisha Mtu aliyeingia mkataba kwenye sekta hiyo  hapati hasara wanatengeneza mwongozo unaofanya ukokotoaji wa mabadiliko ya bei.

Pia amesema kuwa wanatengeneza mwongozo wa vifaa vya Ujenzi ambavyo vinakidhi viwango na vinaweza kutumika kupitia vifaa vya ujenzi na vinakidi mikataba mbalimbali. 

"Tulitengeneza mkataba wa Ujenzi wa majengo tunayo Taasisi ya PPRA ambayo inatenengeneza nyaraka kwa ajili ya ununuzi wa mambo ya sekta ya umma lakini sekta ya ujenzi inawatu wengi Kwenye sekta isiyo ya umma yaani binafsi hivyo tumetengeza mkataba unaowezesha yule mkandarasi Kwenye sekta binafsi awese kuingiq mkataba wakutekeleza majengo"amesema Dkt Mturi

Kuhusu utoaji wa Mafunzo Dkt Mturi amesema kuwa Baraza Hilo limekuwa likitoa Mafunzo Kwa wahandishi wa Ujenzi Ili waweze kuongeza uwezo wa kiufundi katika kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Vilevile Dkt Mturi ameendelea kusema kuwa wanaowaongezea ujuzi wa kimafunzo kwani mpaka Sasa Kwa Mwaka wa fedha wameshafanya Kwa watu 155 ambao wanaweza kusimamia mradi wa aina yeyote wa Ujenzi.

Hata hiyo Mtendaji Huyo amesema Taasisi hiyo itaendelea kushauri na kutoa mwongozo wa taratibu za kufuatwa na wakandarasi Ili majengo yote yanayojengwa yaweze kuwa na ubora unaotakiwa.

0/Post a Comment/Comments