KATA YA KIBAMBA YATEKELEZA PROGRAM YA WANAFUNZI KULA SHULENI.


Wanafunzi wakiwa katika mstari  Kwa ajili ya kupatiwa chakuka
Diwani wa Kata ya Kibamba Manispaa ya Ubungo Peter Kilango akikagua foleni ya wanafunzi wanaokwenda kuwekewa chakula ambacho kimepikwa shuleni hapo.
Makamu Mkuu wa Shule ya Kibweheri aliwaeleza wanahabari manufaa ya Chakula kutolewa kwa wanafunzi shuleni
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwegere aliwaeleza waandishi wa habari namna wanavyotekeleza mpango wa chakula kwa wanafunzi mashuleni.
waandaaji wa chakula kwa ajili ya wanafunzi.
.......................

NA MUSSA KHALID

Imeelezwa kuwa tangu kuanzishwa kwa program ya wanafunzi kula chakula shuleni imesaidia kuongeza taaluma Pamoja na kupunguza utoro Kwa wanafunzi.

Wakizungumza na baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Kibwegere na Kibweheri ziliyopo kata ya Kibamba Manispaa ya Ubungo Mkoani Dar es salaam wameipongeza serikali kwa kuanzisha program kwani imewasaidia kukabiliana na njaa mchana wakati wa masomo.

Aidha wanafunzi hao pia wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi wasiokuwa na uwezo katika shule mbalimbali ili kwa pamoja waweze kunufaika na mpango huo.

"Tunashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu kwa kuona umuhimu wetu wanafunzi kwani sisi kula shuleni inatusaidia kuondokana na njaa lakini pia inatusaidia kuwa taaluma nzuri"wamesema wanafunzi

Kwa upande wao walimu wakuu akiwemo Makamu Mkuu wa Shule ya Kibweheri na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwegere wameipongeza serikali  Kwa kuwaletea mwongozo huo ambao umewasaidia wanafunzi kula shuleni na hivyo kuondokana na changamoto ya utoro wa mara kwa mara kwa wanafunzi.

Walimu Hao wamewashauri wazazi na walezi kuhakikisha wanawapatia watoto wao Fedha za chakula 5000 Kwa wiki Ili waweze kula kama wanafunzi wenzao ambao wanalipiwa.

Akizungumza mafanikio ya program hiyo ya Chakula shuleni,Diwani wa Kata ya Kibamba Manispaa ya Ubungo Peter Kilango amesema wanafunzi wanaotoka mbali na kukaa muda mrefu shuleni.

Hata hivyo Diwani Kilango amewasisitiza kuwa wataendelea kufanya vikao na wazazi Ili kuangalia utaratibu Mzuri wa kuwalipia wanafunzi kwani baadhi wamekuwa na changamoto ya kupewa pesa lakini hawalipi Shuleni.

0/Post a Comment/Comments