KATA YA NDUGUMBI YAJIIMARISHA KIMAENDELEO.


Diwani wa Kata ya Ndugumbi Thadey Massawe akizungumza kuelezea miradi ambayo inatekelezwa katika kata hiyo ukiwemo Ujenzi wa Barabara.
Moja ya barabara inayojengwa katika Kata ya Ndugumbi.

...................,........

NA MUSSA KHALID

Wakazi wa Kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam wameupongeza uongozi wa Kata hiyo kwa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuwa katika kiwango cha lami.

Wakizungumza na Kituo hiki kwa Nyakati tofauti wananchi hao wa Kata ya Ndugumbi wamesema kuwa kabla ya ujenzi wa barabara hizo wamekuwa wakikumbana na adha hasa kipindi cha mvua.

Wamesema barabara zinazotengezwa katika kata hiyo zinakwenda kuonyesha ubora wa mitaa yao na hivyo kusaidia kuepukana na changamoto ambazo wamekuwa nazo kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ndugumbi Thadey Massawe amesema ujengaji wa barabara hizo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambapo mpaka mwaka huu zitakuwa zimekamilika.

"Tunatekeza miradi hii ya Barabara kama tulivyowaahidi wananchi wakati wa Kampeni za Uchaguzi hivyo nawasihi waendelee kuwa bega kwa nasi Ili tuendelee kufanikisha kwa wakati miradi mbalimbali ambayo tunaitekeleza" amesema Diwani Masawe

Katika Hatua nyingine Diwani Massawe amesema pia wamefanikia kutatua kero ya muda mrefu iliyokuwa inawakabili wananchi wake katika Mto Ng’ombe nyakati za mvua wameimarisha na kuiboresha mitaro ili maji yaweze kupita.

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa walinzi wa kutunza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali yao ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira yao kwa kuepuka kutupa taka hovyo ili yaweze kuwa katika hali ya usafi.

Diwani Masawe ameendelea kusema kuwa ataendelea kushirikiana na wenyeviti na Viongozi mbalimbali ndani ya kata hiyo Ili waweze kutekeleza Kwa Pamoja miradi mbalimbali ya kimkakati.

0/Post a Comment/Comments