MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU WA SMZ NA JMT WAWASILI ROMA KWA MKUTANO MKUU WA IFAD

 


Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa viongozi waandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Uvuvi, Mashimba Ndaki (wa kwanza kulia kwa Balozi)Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na.Mwandishi Wetu,

Roma, Italy.

VIONGOZI waandamizi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wakiwemo Makatibu Wakuu wawili na Mawaziri wawili wamewasili mjini hapa Roma tayari kushiriki katika Baraza Kuu la Mfuko wa Maendeleo ya Chakula na Kilimo duniani IFAD unaotarajiwa kuanza Februari 13,2023.

Ujumbe huo mzito kutoka Wizara za Uvuvi na Mifugo, pamoja na ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ukiongozwa na Waziri wa mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki ambaye ni Mkuu wa msafara huo unatarajiwa kuwakilisha vyema Serikali katika mambo mtambuka ya uvuvi

Aidha, tayari ujumbe huo umepokelewa na Mhe. Balozi wa Tanzania nchini Italia, Balozi Mahmmoud Thabiti Kombo pamoja na Maafisa wa Ubalozi huo wakiongozwa na Mwambata wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Misitu Bi.Jacquiline Mbuya Mhando.

Mwisho.

0/Post a Comment/Comments