Imeelezwa
kwamba, mfumo unaotumika kusambaza mbolea za ruzuku umesaidia kuondoa biashara haramu ( black
market) ya mbolea na kupunguza ushindani
kwenye soko la ndani kufuatia bei ya bidhaa hiyo kwa wakulima kuwa ni moja nchi
nzima.
Hayo
yamebainishwa na Meneja wa Mauzo wa kampuni la mbolea la Mohamed Enterprise
Kanda ya Kaskazini, Jafar Abbas alipokuwa akizungumza na wanahabari waliofika
lilipo ghala la mbolea ya kampuni hiyo Jijini Arusha.
"Mfumo
umeondoa biashara ya magendo na tabia za watu kuhodhi mbolea ili baadaye wauze
kwa bei ya juu" Abbas anasisitiza.
Amesema,
mfumo huo pia umewasaidia wafanyabiashara na serikali kwa ujumla kupata takwimu
sahihi za kiasi cha mbolea kilichouzwa kwa wakulima na kiasi kilichopo kwa
ajili ya usambazaji.
Aidha,
Abbas ameeleza kuwa, mfumo wa mbolea ya ruzuku umewasaidia wakulima kununua
bidhaa hiyo kwa bei halali tofauti na awali ambapo kila mfanyabiashara aliuza
bei yake ilimradi alizingatia bei elekezi iliyotolewa na serikali kupitia
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, (TFRA).
Kwa
upande wake Richard Kika Afisa Masoko wa
Mohamed Interprise tawi la Arusha
amesema awali kampuni lao lilikuwa likiuza mbolea Jijini Dar es Salaam
na wamefungua matawi mengine hususani la Arusha Mwezi September, 2022.
Aliongeza
kuwa, kiasi cha mbolea kilichouzwa mpaka mwishoni mwa mwezi Januari, 2023 ni
tani 782 ambapo msimu wa kilimo mkoani humo bado haujaanza na kubakiwa na mifuko 623 ya mbolea
ghalani huku wakitarajia kuongeza mauzo kutokana na mwitikio wa wakulima wa
kutumia mbolea msimu huu wa kilimo.
Ameeleza kuwa, bado mbolea nyingine inaendelea kuletwa ili kukidhi mahitaji ya wakulima kwa msimu wa kilimo unaoanza mwezi Februari kwa mikoa ya Kaskazini.


Post a Comment