NMT YAENDELEA KUSISITIZA JAMII KUFANYA UTALII WA NDANI.





......................

Na Mwandishi wetu

Afisa elimu mwandamizi Mkumbusho ya Taifa Anamery Bageny amewataka Watanzania kuendelea kujiwekea tabia ya kufanya utalii katika maeneo mbalimbali nchini ili wajifunze urithi wa nchi yao.

Bageny amesema hayo jijini Dar es salaam katika ziara maalum ya utalii ya katika program ya Museum University Hub ambayo imeandaliwa na Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma taaluma ya urithi wa utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Amesema kuwa jamii imekuwa na mazoea ya kudhani kufanya utalii ni kwenye mbuga za wanyama maeneo tengefu hivyo ni vyema pia wakajikita katika kufanya utalii wa kiutamaduni ukiwemo wa jiji.

‘Tunawapa wanafunzi nafasi ya kulitazama jiji la Dar es salaam kwa jicho la utalii kwa sababu wamekuwa wakipita katika maeneo hayo wakielekea katika maeneo mbalimbali kwani Makumbusho tumekuwa tukiifungua Dar es salaam ili kuhakikisha watalii wanaongezeka kwa wingi’amesema Bageny

Amesema malengo yao pia ni kuhakikisha wanawaelimisha watanzania kuhusu kufanya utalii wa kiutamaduni ikiwa ni pamoja na kujifunza urithi uliopo kwenye nchi yao.

Aidha Bageny amewasisitiza watanzania kuendelea kutoa nafasi kwenye utalii wa kiutamaduni hasa unaopatikana katika jiji la Dar es salaam ili waendelee kuuza mji huo.

Bageny ameyataja baadhi ya maeneo ya kiutalii katika jiji la Dar es salaam kuwa ni pamoja na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni,Kijiji cha Makumbusho,Soko la samaki feri,Mnara wa askari pamoja na Magofu ya Kunduchi.

Naye Muhifadhi Mkuu Daraja la kwanza Malikale na Kamanda wa Kituo cha Mgofu ya Kale Kunduchi amezipongeza taasisi mbalimbali kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha utalii wa ndani.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi na wadau ambao wameshiriki katika kufanya utalii huo wamesema kuwa wamejifunza mambo mengi ya kihistoria hivyo watakuwa wajumbe wa kuishawishi jamii kujifunza na urithi wan chi.

0/Post a Comment/Comments