Naibu Katibu Mkuu wizara ya uwekezaji, viwanda na Biashara Bwana Ally Gugu akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara Nchini -TNBC, Dkt Godowill Wanga akinena na wanahabari Jijini Dar es salaam.

Waandishi wa Habari wakifatilia hotuba ya Viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wizara ya uwekezaji viwanda na Biashara Bwana Ally Gugu.
Na: Issa Mohamed
Email: issahmohamedtz@gmail.com
Naibu katibu Mkuu wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara Ally Gugu amewataka wadau wa sekta binafsi kutoa mapendekezo ya maboresho ya sheria katika sekta ya uwekezaji ili kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikumbuka sekta hiyo.
Ametoa kauli hiyo wakati wa kuelekea mkutano unaotarajia kufanyika Februari 2 Jijini Dar es salaam na kujumuisha sekta ya Umma na Binafsi lengo ni kuleta majadiliano ya pamoja katika sekta ya Uwekezaji na Biashara kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa.
Amesema serikali imeendelea kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa miundominu ikiwemo Gesi Asilia, Ujenzi wa reli, banadari ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa hizo.
‘’Mkutano huu ni wa sekta ambao unahusisha wadau wa sekta ya uwekezaji, viwanda na biashara ambapo tutapata fursa ya kujadiliana pamoja na kujadiliana kwa maendeleo mapana ya Taifa letu’’ Amesema Bwana Gugu.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la biashara –TNBC, Dkt Godwill Wanga amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kujadili sheria na kanuni za biashara ili kuwa na sheria rafiki za uwekezaji kwa sekta binafsi.
‘’Na hapo tunaangalia sheria na kanuni zinazohusu biashara ili kufikia pale ambapo tumekusudia, uchumi ukishakua kila kitu kinashuka ikiwemo riba na mfumuko wa bei za bidhaa muhimu’’ Ameeleza Dkt Wanga.
Naye Mkurugenzi wa bodi ya Taasisi ya sekta binafsi –TPSF, Octavian Mshiu ameishahuri serikali kuhakikisha inaleta mjadala mpana kuhusu gesi asilia kutokana na kua na uhitaji mkubwa katika soko la Dunia.
‘’Tunatambua kuwa Taifa letu linaenda kuwa katika uchumi mkubwa wa gesi kutokana na mahitaji ya Gesi Duniani yameongezeka kama Taifa lazima tujadili kwa kina ili kuwa wauzaji wakubwa wa Gesi Duniani’’ Amebainisha Ndugu Mshiu.
Mkutano huo umebebwa na kauli mbiu isemayo ‘’Uboreshaji wa mzingira ya Biashara na Uwekezaji kwa maendeleo ya Uchumi wa Tanzania’’ na unatarajia kushirikisha wadau zaidi ya 500 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
MWISHO


Post a Comment