Kaimu
Meneja Kitengo cha Tathmini ya viatarishi vya Chakula TBS Ashura Katunzi
Kilewela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
.........................
NA
MUSSA KHALID
Shirika
la Viwango Tanzania –TBS limewasisitiza watanzania kuzingatia kanuni tano za
usafi na ulaji wa chakula salama ili kuweza kuepukana na madhara yanayotokana
na kutokula chakula salama.
Pia
imeelezwa kuwa ili mwananchi kuwa na chakula toshelevu ni vyema akawa na
chakula salama katika kaya ambacho maandalizi yake yanaanzia shambani.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Meneja Kitengo cha Tathmini ya
viatarishi vya Chakula TBS Ashura Katunzi Kilewela ambapo amesema kuwa ni vyema
jamii ikazingatia kanuni tano za kuwa na chakula salama ikiwa ni pamoja na
kuzingatia usafi.
Aidha
ameitaja kanuni nyingine kuwa chakula kinapaswa kupikwa mpaka kiive ili kuondoa
uwezekano wa vimelea vya magonjwa kuweza kumdhuru mtumiaji.
‘Tunaposema
usafi kwa wakati huu kuna kuwa na maandalizi ili wanakaya waweze kukila hicho
chakula kuanzia namna ambavyo unakiosha au vyombo ambavyo unavitumia katika
maeneo mbalimbali ikiwemo kwa mama lishe ni muhimu kuzingatia suala la usafi’amesema
Kilewela
Kanuni
nyingine amesema ni muhimu kuitenganisha chakula kilichopikwa na kibichi ili
kama kunauchafuzi wowote kwenye chakula kibichi au vimelea vya magonjwa isije
ikahatarisha kilichopikwa na kukosa usalama.
Wakizungumza
na kituo hiki baadhi ya waandaji wa chakula wamesema wamekuwa wakizingatia
usafi wa chakula kabla na baada ya kuwapatia walaji jambo huku wakiwashauri
waandaaji wengine wa chakula kutokujisahau.
Hata hiyo Kilelewa amesema wataendelea kushirikiana na watendaji wengine kwenye kata wakiwemo maafisa ugani na afya kwa kutoa mafunzo ili elimu ifike na kuhakikisha mlaji anapata chakula kilichobora na salama.

Post a Comment