Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu akitembelea Banda la COSTECH katika Maadhimisho ya siku ya uwekezaji ambayo yameratibiwa na CRDB
.................
NA MUSSA KHALID
Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imeshiriki katika Maadhimisho wa siku ya uwekezaji wenye lengo la kutoa Maarifa kwa vijana kuhusu kuwa wabunifu katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali.
Katika Mkutano Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, COSTECH imekwenda na kauli Mbiu isemayo Taifa linaongozwa na Sayansi,Teknolojia na Ubunifu
Mtoa mada katika Mkutano huo wa siku ya uwekezaji ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu.
Katika Mkutano huo COSTECH inashiriki ikiwa ni katika kuendeleza makubaliano waliyoingia kupitia hati ya makubaliano iliyosainiwa tarehe 20 Februari 2023 ili kuruhusu mchango wa sekta binafsi za kifedha na CRDB kupitia mpango wezeshi wa IMBEJU unaolenga kuwezesha vijana na wanawake kuwapatia mitaji ya ubunifu
Pia COSTECH inashiriki kama mtaalamu wa (technical support) ya kufanyia tathimini ya maombi ya wabunifu ili kuwakabidhi wabunifu kwa benki ya biashara ya CRDB
Afisa Habari wa Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH Feisal Jalil akiwaeleza wadau waliotembelea katika banda lao kwenye Mkutano huo unaofanyika Kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa JNICC uliopo jijini Dar es salaam 

Mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa kilimo TARI-Mikocheni Margareth Daudi Lupembe akimueleza mdau aliyetembelea katika Banda lao kumuonyesha namna wanavyofanya utafiti.






Post a Comment