
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akishuhudia utiaji saini wa makubalino
ya awali ya ujenzi wa kiwanda cha saruji kitakachokuwa na uwezo
wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka katika Wilaya ya Kongwa.
Makubaliano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki kati ya kampuni yaAlotab &
Block BB na Libyan Petrolium ya Libya. Hafla hiyo
imefanyika mbele ya wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Dodoma jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa
Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) na Mwenyekiti wa
Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab (kulia) wakibadilishana hati
za makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha saruji Mkoani Kongwa.
Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini
wa makubalino ya awali ya ujenzi wa
kiwanda cha saruji kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni
moja kwa mwaka katika Wilaya ya Kongwa. Uwekezaji wa Kiwanda hicho utagharimu
dola za kimarekani milioni mia mbili. Kiwanda hicho kitasaidia kuleta ajira na kuinua pato la mkoa na Taifa kwa
ujumla.
*************************************************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule jana
17 Machi 2023 ameshuhudia utiajia saini wa makubaliano ya awali ya ujenzi wa
kiwanda cha saruji ambacho uwekezaji wake ni wa thamani ya Dola Milioni 200.
Makubaliano hayo
yamefanyika kati ya kampuni ya Alotab & Block
BB na Libyan Petrolium ya Libya ambapo kiwanda
hicho kinatarajiwa kujengwa Wilayani Kongwa. Hafla hiyo imefanyika mbele ya wajumbe wa Baraza la
Ushauri Mkoa wa Dodoma jijini Dodoma.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewahakikishia wawekezaji hao
mazingira rafiki ya kutekeleza shughuli zao za uwekezaji na kuwakaribisha
kuwekeza zaidi katika ujenzi wa viwanda vingine.
“Nawakaribisha
Dodoma, Makao Makuu ya Nchi yetu, fursa za uwekezaji ni nyingi wekezeni zaidi katika
Mkoa wetu, tunayo ardhi na malighafi ya kutosha” Senyamule alisisitiza.
Nae Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt Omary Nkullo amesema katika Wilaya yake
ekari 500 zimepimwa katika eneo la Pandambili maalumu kwa ajili ya uwekezaji.
Hatahivyo Bw
Anyid Dmjed Rajab wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libra amesema
wataendelea kuwekeza katika maeneo mengine katika Mkoa wa Dodoma kutokana na mazingira
rafiki ya uwekezaji na upatikanaji wa malighafi.
Post a Comment