Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Naibu Waziri wa
Masuala ya Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Estonia Mhe. Marjin Ratnik
walipokutana na kufanya mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi
zinazoendelea za kipato cha chini, mjini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Naibu Waziri wa Masuala ya Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Estonia Mhe. Marjin Ratnik, kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, walipokutana na kufanya mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato cha chini, mjini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Naibu Waziri wa
Masuala ya Uchumi na Maendeleo wa Serikali ya Estonia Mhe. Marjin Ratnik baada
ya kumaliza kufanya mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi
zinazoendelea za kipato cha chini, mjini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akizungumza na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe.
Chrysoula Zacharopoulou walipokutana
na kufanya mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi
zinazoendelea za kipato cha chini mjini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Ufaransa Mheshimiwa Chrysoula Zacharopoulou walipokutana
na kufanya mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi
zinazoendelea za kipato cha chini mjini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe.
Chrysoula Zacharopoulou, akizungumza na Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), walipokutana na kufanya
mazungumzo kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea za kipato
cha chini, mjini Doha nchini Qatar.
(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, WFM, Doha, Qatar)
..............
Na. Josephine Majura (WFM), Doha Qatar
Serikali ya Estonia imeahidi kuisaidia
Tanzania kuboresha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya
ukusanyaji kodi ili kusaidia kupiga hatua zaidi katika masuala ya usimazi wa
kodi na kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa
Masuala ya Uchumi na Maendeleo wa Estonia, Mhe. Marjin Ratnik, alipofanya
mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
(Mb), mjini Doha, Qatar, kando ya Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi
zinazoendelea za kipato cha chini unaoendelea nchini humo.
Mhe. Ratnik alisema Serikali yake ipo
tayari kuwapokea wataalamu kutoka Tanzania kupata mafunzo ya mifumo ya tehama
ya ukusanyaji kodi nchini humo kwa vitendo ili wapate utaalam
utakaowasaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Serikali imepokea rasmi
mwaliko wa kuwapeleka wataalamu wa Tanzania kupata mafunzo hivyo wameanza
maandalizi ya safari hiyo ambapo mwezi Mei mwaka huu wataalam wanaohusika na
masuala ya ukusanyaji kodi watakwenda nchini Estonia kujifunza mifumo
mbalimbali ya ukusanyaji kodi.
“Juhudi hizi ni utekelezaji wa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, la
kuboresha mifumo ya kodi ili kuwepo na uwazi katika ukusanyaji”, alisema Dkt.
Mwigulu.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Wizara
ya Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa kuwepo
kwa mifumo bora ya ukusanyaji kodi itaongeza uwajibikaji wa watalaam
wanaohusika na ukusanyaji kodi.
Aliongeza pia kuwepo kwa mifumo ya
pamoja ya ukusanyaji kodi itamsaidia mlipakodi kulipa kodi mara moja katika
Taasisi zote zinazohitaji kufanya hivyo.
Katika tukio jingine Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alikutana na kufanya mazungumzo
na Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Ufaransa, Mhe. Chrysoula Zacharopoulou ambapo Waziri huyo
alisema Serikali yake ipo tayari kusaidiana na Tanzania katika ujenzi wa
bandari itakayohudumia Tanzania na nchi jirani
“Ufaransa ipo tayari pia kutusaidia kukuza
sekta binafsi ambayo imekuwa ikitoa ajira nyingi kwa vijana nchini”, alisema
Dkt. Nchemba.
Aliongeza kuwa Serikali ya Ufaransa itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuboresha miundombinu ya barabara, nishati na
umeme wa jua ili iweze kutumika katika shughuli za uzajilishaji.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na
Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, alisema kuwa Ufaransa
imetangaza rasmi kushirikiana na Tanzania katika kukuza sekta ya utalii
kwa kuwa ina mchango katika pato la Taifa.
Aliongeza kuwa Serikali ya Ufaransa imekuwa
ikiisaidia Zanzibar katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo
miundombinu, afya na nishati.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou, alisema kuwa pamoja na ushirikiano
mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa, anaamini kuwa bado kuna mengi zaidi
ya kushirikiana kati ya nchi hizo mbili.
Mhe. Zacharopoulou alipongeza msimamo wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye masuala ya jinsia na nia ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jukwaa la Usawa wa Kizazi (Generation Equality Forum) baadae mwaka huu.
.jpg)
.jpg)
.jpg)



Post a Comment