FRIENDS OF TULIA TRUST WACHEZEA KICHAPO KWA ESPANYOL

 

*****************************

TIMU ya Friends of Tulia trust wayaaga Mashindano rasmi kwa upande wa Wanawake na  Wanaume kutokana na kipigo kikali kutoka timu ya Espanyol. 

Akizungumza Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa amesema Mchezo huo wa Sodo 4 Climate  una lenga zaidi kuhamasisha Mazingira kuwekwa safi hususani maeneo ya Fukwe za Bahari.

"Lengo la Mchezo wa Sodo 4 Climate ni kukumbusha jamii kufanya usafi na kutunza Mazingira ya Fukwe za bahari ambapo ligi hii inaendelea kufanyika maeneo ya Fukwe hizi za Coco Beach. 

Rugambwa ameeleza kuwa Mchezo huo  kati ya Friends of Tulia trust dhidi ya Espanyol zilihusisha upande wa Timu ya Wanawake na Wanaume. 

" Sodo upande wa wanawake Friends of tulia 1-2 Espanyol, katika sodo wanaume friends of Tulia Trust 0-2 Espanyol. Hivyo Friends of tulia trust tayari wameaga mashindano rasmi ".

0/Post a Comment/Comments