GARI LILILOBEBA GESI LAUA WATATU HANDENI TANGA.

 

***************

Na Richard Mrusha Handeni 

WATU watatu wa familia ya Mzee Amri Nyundo wa Kijiji cha Kwamwachalima ,kata ya Kwamkonga wilaya ya Handeni  mkoani Tanga wamepoteza maisha na watu wengine nane wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya  Bombo mkoani humo Kwa ajali ya moto uliotokana na Lori lililobeba gesi kudondoka na kulipuka.

Akithibitisha kutokea Kwa ajali hiyo leo Machi 31 mbele ya waandishi wa Habari  mkuu wa Wilaya hiyo Albert Msando Amesema nikweli ajali hiyo imetokea na  imesababisha vifo vya watu watatu kutoka familia Moja lakini na watu wengine nane wamejeruhiwa Kwa asilimia 90 na hali zao mbaya sana.

Amesema ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo saa 11 ambapo Lori lililokuwa limebeba gesi kutoka Dar es Salaam  na kuelekea Nairobi Kenya,kwakile kilichodaiwa   kupasuka taili moja kisha kudondoka  na kulipuka kwa moto,  kuanza kusambaa kwenye makazi ya watu na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umeme.

" Kama mnavyoona hapa ndugu waandishi wa Habari hii ni ajali iliyotokana na moto wa gesi ambapo watu watatu wa familia Moja kufariki dunia na  Kati yao watoto wawili na mama  yao wote wamepoteza maisha."amesema Mkuu wa Wilaya Msando 

Nakufafanua kuwa " mama huyo amepoteza maisha akiwa katika harakati za kuwaokoa watoto wake ambao walikuwa wamelala ndani ya nyumba yao. Sisi kama  Serikali tumebeba msiba huu na tumekwenda kuzika katika Kijiji cha jirani na majeruhi wote nane wamelazwa katika Hospitali ya Bombo  na Serikali inashughulikia matibabu yao."Amesema Msonda

Katika hatua nyingine mkuu wa Wilaya huyo  amefafanua kuwa kutokana na ajali hiyo pia  imeharibu miundombinu ya umeme  ikiwamo nguzo zake kuungua ambapo  Tanesco pamoja na vyombo vya Dora wapo katika eneo hilo la tukio  kuhakikisha wanarejesha Kwa miundombinu iliyoharibika.

Pia amewashukuru wananchi wa kata hiyo na Kijiji cha kwamwachalima Kwa ushirikiano walioonyesha mara baada ya kutokea Kwa ajali hiyo nakwamba  walishirikiana kikamilifu na Jeshi la Zima moto na uokoaji kuhakikisha wanadhibiti Kwa haraka kusambaa Kwa moto huo.

Naye Habiba Omari na Ibrahimu Abdallah ni mashuhuda wa ajali hiyo na wakazi wa Kijiji hicho  wamesema kuwa walisikia kishindo kikubwa barabarani  baada ya kutoka nje ndipo walipoona Lori kubwa lililokuwa limebeba gesi lilokuwa likitoka Dar es Salaam likiwa limepinduka na kulipuka.

 Wamesema kuwa kutoka na ajali hiyo imesababisha vifo hivyo vya watu watatu ambao wote wametoka kwenye familia ya mzee Amri Nyundo ambaye ni Mume wa mama aliyefariki ambapo hata hivyo Yeye yupo safarini Dar es salaam..

Mwisho

0/Post a Comment/Comments