KATIBU MKUU NDUNGURU AKABIDHIWA OFISI RASMI





Na. Asila Twaha, OR- TAMISEMI

Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Adolf Ndunguru amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Prof. Riziki Shemdoe ambaye sasa ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Makabidhiano hayo yamefanyika  Machi 06, 2023 kwenye Ofisi ya Rais iliyopo katika Mji wa Serikali Mtumba na kushuhudiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara hiyo.

Aidha, amewashukuru menejimenti kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichoongoza Wizara hiyo na amewaomba watumishi hao kuendelea kutoa ushirikiano na kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu kwa viongozi hao  walioteuliwa lengo likiwa kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Katibu, Mkuu Ndugu Adolf Ndunguru amemshukuru Prof. Riziki Shemdoe na kumuahidi  kuyaendeleza yote  aliyompatia ili wananchi waendelee kuwa na imani na Wizara hiyo na kuwa atafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na ubunifu.

“Ninakushukuru kwa kunikabidhi  ofisi nitaendeleza yale ambayo umeniachia na mbali  ya  haya yaliyoandikwa humu kwenye vitabu lakini  pia nikiwa na jambo la kukuuliza nitakuja mwenye kukuona ili unipe mwongozo zaidi” Ndunguru

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshuhulikia  afya Dkt. Grace Magembe ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

0/Post a Comment/Comments