KLABU YA SIMBA NA MOBI AD YAINGIA MAKUBALIANO YA UENDELEZAJI VIPAJI KWA VIJANA

 





                                   **************

Timothy Marko 

KATIKA  kuhakikisha sekta ya Michezo inakuwa hapa nchini klabu ya simba imeanzisha program maalum yakuwa kuza wachezaji vijana kisoka .

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam  Mkurugenzi wa timu hiyo Imani kajura amesema kuwa program hiyo itakayo gharimu shilingi miioni 500 .

"Program hii inayoitwa the future is now inalenga kuwa kusanya vijana wenye vipaji vya mpira"Alisema Mkurugenzi Imani kajura .

Kajura alisema sambamba undelezaji wa vijana  kimichezo pia Programu hiyo inalenga pia kuwaendeleza vijana hao kielimu.

Alisema mfumo huo wakuwakusanya vijana  katika kuendeleza kisoka utakuwa ni wauwazi.

Naye Mtendaji wa kampuni  ya Mobiad Rumisho Sikoni amesema kuwa kampuni  hiyo inakusudia kuipa shillingi milioni 500 klabu ya simba kamafedha yauendelezaji wa Program miaka miwili.

Alisema mfumo huo wa kuwaendeleza vijana umeweza kuwasaidia wachezaji kama vile Said Ndemla Ibrahim  Ajibu.

0/Post a Comment/Comments