SERIKALI YAWATAKA WADAU WA SEKTA YA ELIMU KUTOA ELIMU INAYOZINGATIA MAADILI MEMA KWA JAMII .


...................


Timothy Marko

SERIKALI imewataka wadau  wa sekta ya Elimu kuzingatia ufundishaji wa masuala ya Maadili kwa wanafunzi shuleni ili kujenga Jamii inayozingatia maadili mema kwa Jamii navizazi vijavyo.

Akizungumza9 katika uzinduzi wa mpango Mkakati wa uboreshwaji wa sekta hiyo ya mwaka 2023 January Hadi Disemba 2027 ya taasisi ya Ten Met mapema hii Leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa Elimu kutoka wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia Ephraim Sembeye amesema kuwa  nimuhimu kwa watoto mashuleni wa kafunzwa maadili mema nakuondokana natatizo la watoto kuimba nyimbo zisizo zingatia maadili ya kitanzania .

"Nimeshuhudia Watoto wakiimba nyimbo za ajabu kwenye Mabasi Hali iliyoleta taharuki kwa jamii iliyopo kwenye mabasi".Alisema Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa Elimu Ephraimu Sembeye.

Sembeye amesema kuwaserikali imekuwa ikifanya mabadiliko ya sera ya Elimu kwa kuzingatia mabadiliko katika sekta ya ajira kwa kushirikiana na asasi za kirahia .

Alisema pamoja na Asasi nyingi kuweka vipaumbele katika masuala ya ukatili wa kijinsia ni muhimu kwa asasi hizo kupigia mbiu katika kuboresha sekta ya Elimu nchini.

"Asasi za kirahia ni wadau muhimu katika kupinga ukatili wa kijinsia, sasa nimuhimu kwa asasi za kirahia kugeukia kupigia mbiu masuala yaubora wa Elimu ".Aliongeza Sembeye. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mtandao wa Elimu Tanzania (Ten MeT)Faraja  Naylandu amesema kuwa kutokana nakuwepo kwa Janga la Uviko 19 kumeleta changamoto ya kujifunza kwa watoto hali inayochangia kushusha morali ya watoto kujifunza .

Alisema uzinduzi wa mpango wa mapendekezo wa mabadiliko ya sera ya Elimu kutaleta chachu ya Mabadiliko katika sekta ya Elimu.

0/Post a Comment/Comments