SHULE YA ALPHA YAZINDUA MFUMO WA KUPIMA VIPAJI KWA WATOTO

Mratibu wa Mtaala wa ziada wa shule ya sekondari ya Alpha bwana Fulgence Kabiligi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashine ya kupima vipaji

 ......................

Na Richard Mrusha 

Kwa mara ya Kwanza nchini Mfumo wa kupima vipaji kwa watoto umezinduliwa rasmi katika Shule ya Sekondari ya Alpha iliyopo jijini Dar es Salaam. 

Mfumo huo utahusika kupima vipaji vya watoto kijidigitali ili kuweza kusaidia watoto kuelekezwa katika vipaji vyao na kuvitumikia ipasavyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Profesa wa sheria na mtoa mihadhara maarufu kutoka Kenya Patrick Lumumba alisema watasambaza ujumbe huo mzuri kuwa shule za Alpha ndio zimechaguliwa kuwa kitovu anzilishi kuwa na mfumo huo mpya ambao utakuwa na manufaa kwa vijana wa kitanzania wa kike na kiume na Afrika pia.

Prof Lumumba alieleza kuwa kupitia mfumo huo vijana watakaotambulika vipaji vyao watawezeshwa ili mafanikio yao yasikwazwe bali yapewa rutuba.

"Kupitia mfumo huo mtoto atapimwa kipaji chake na kusaidiwa kutumia vizuri kwani kila mtu anakipaji ila wengine hawajui hivyo hawataweza kutumia ipasavyo kwakuwa teknolojia sasa ndio kitu muhimu Duniani,"alisisitiza Prof Lumumba. 

Kwa upande wake Mratibu wa Mtaala waziada wa shule ya Alpha sekondari,Bwana Fulgence Kabiligi alisema shule hiyo imejikita kugundua vipaji mapema kabla ya mashine hiyo kwa kuanzisha vilabu 21 na kufundisha jinsi ya kuwa wajasiriamali.

"Hii mashine ni kwa ajili ya watanzania wote kwahiyo tupo wa aina nyingi wenye uwezo mkubwa.,mdogo na ambaoa hawana watatafutiwa utaratibu.

Alisema Manufaa yake inamsaidia kupima kipaji na kukijua na kuendelezwa katik shule ya kipaji husika na kusoma kwa haraka na muda mfupi ili kuweza kutumia kipaji chake. 

"Mtoto anapimwa kwa mwanasaikolojia kujua historii yake , asili na anapendelea nini baadae anaingia kwenye mashine inachukua vina saba na wanatoa michoro ambayo inatumwa mtandaoni Jeniva wao wanasoma na kurudisha majibu ndani ya dakika chache,"alieleza Kabaligi.

Alifafanua kuwa watakuwa na kliniki zitakazoendeleza vipaji na pia vyuo na watashirikiana na shirikisho la vipaji Duniani na katika kupima wakigundua Duniani vipaji hivyo ni vichache atachukuliwa kwenda nje kwa lengo la kuendelezwa.

Alieleza kuwa Mashine hiyo ni kamera ya kawaida haina mionzi wala mdhara inapima neva zinaelekea wapi kwa wingi.

"Tutaweka uratibu wa kupima kwa watu ambao hawana uwezo tutatumia serikali za mitaa na tutatumia pia utaratibu kulingana na taratibu za shirikisho la vipaji Duniani na kliniki zitakuwa na gharama kidogo tutashirikiana na serikali,"alisisitiza. 

Naye Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Abdul Maulid alisema ikiwa watoto watapimwa kupitia mfumo huo itarahisisha kwani wapo wazazi wanawalazimisha watoto kubeba vipaji vyao hivyo ikijulikana atapelekwa anapostahili.

Alisema wao wanatumia waalimu kugundua vipaji vya watoto kutokana na elimu walizopatiwa kwa muda mrefu.

"Tulikuwa tunajua kuwa huyu mwanafunzi anafaa kusom sayansi,huyu biashara na huyu masomo ya Sanaa hivyo tuna kazi hiyo mfumo huo utaondoa shida kwa mzazi kutaka mtoto wake kuwa kama yeye atafata kipaji chake ,"alisisitiz

0/Post a Comment/Comments