TANZANIA KUHESHIMU MIKATABA YA KIMATAIFA YA KAZI NA AJIRA

 


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi akifungua Warsha hiyo iliyofanyika Jijiji Dar es salaam

Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  Suzanne Ndomba
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri Paul Sangeze.

*****************

Timothy Marko

Serikali  imesema itaendelea kuheshimu mikataba ya Kimataifa kwa kuhakikisha inaweka ulinzi mahali pa kazi ili kusaidia  Ustawi wa Jamii yenye uchumi Imara 

Ameyasema hayo Leo Jijini Dar es salaam Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku Moja kuimarisha Uhusiano Bora kati ya Chama chama Cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara ,Taasisi za fedha huduma na ushauri(TUICO) ambapo amesema Serikali inapenda sekta zote za kazi kwani zina mchango mkubwa kuongeza Pato la Taifa.

Waziri hii ya leo itakuwa chachu ya kiungo muhimu cha ushirikiano wa Waajiri,Wafanyakazi pamoja na taasisi za kifedha katika kutekeleza Maadhimio ya Shirika la kazi Duniani ILO ili kuboresha mazingira rafiki katika eneo la kazi"amesema Waziri

Hata hivyo Waziri amewaasa kutotumia wanasiasa katika vyama vyao vya kazi kwani hapo awali baadhi yao wametumia vyama hivyo kwa ajili ya maslahi yao ya kisiasa hivyo kupitia Warsha hii ya leo iwasaidie kuzungumza pamoja changamoto zenu na kuzitatua pasipo kupitia kwa wanasiasa

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda biashara,taasisi za fedha ,huduma na Ushauri Paul Sangeze amesema Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi waandamizi waliohudhuria itakuwa chachu yale yatatakayojadiliwa italeta tija kwa kwa kuboresha mazingira mahala pa kazi.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  Suzanne Naomba amesema Waajiri haki ya kujiunga na Chama Cha Wafanyakazi ipo kikatiba mtu binafsi hashurutishwi anajiunga kwa hiari yake mwenyewe na anatakiwa afuate utaratibu..

Aidha Waajiri ni Wadau wakubwa hivyo ushirikiano huo utasaidia kutatua changamoto mahala pa kazi hivyo ni vyema mikaba yote yote ya kazi ifanyike kwa uwazi na majadiliano yafanyike Kwa Nia njema pande zote waridhike

0/Post a Comment/Comments