************
Timothy Marko
KATIKA Kuhakikisha ushiriki wa Wanawake Katika Biashara, Chama Cha Wanawake wenye Viwanda na Biashara TWCC kimeaandaa tunzo za Viwanda ilikuweza kuchochea Maendeleo katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar Salaam Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake wenye Viwanda nchini Mwjumuma Mwajuma Hamza amesema kuwa Wanawake wamekuwa nguzo Muhimu katika maendeleo hasa katika Viwanda.
"Wanawake wanaweza kufanya Mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Viwanda endapo wataaminiwa nakupewa nafasi". Alisema Mkurugenzi wa Twcc Mwajuma Hamza.
Mwajuma Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwezesha Mazingira ya Biashara kwa Wanawake. Katika uanzishwaji wa Biashara.
Aliongeza kuwa taasisi hiyo inampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha Mazingira ya Uwekezaji nchini.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Trade Mark nchini Monica Hangi amesema kuwa Shirika Hilo limetenga zaidi ya shilingi Billion nneilikuweza kufanikisha Miradi Mbalimbali ya kuwajengea uwezo Wanawake.
"Tunzo hizi zinalengo lakuhakikisha Biashara za Wanawake nchini zinakuwa nakuleta tija kwa taifa". Alisema Monica Hangi.


Post a Comment