WAKAAZI WA MAGOMENI KOTA WATAKIWA KUDUMISHA USAFI KWENYE MAKAAZI YAO.

........................

Na.Timothy Marko.

Wananchi wametakiwa kudumisha usafi katika maeneo ya makazi ya mradi wa nyumba za kisasa za Shirika la nyumba la taifa zilizopo eneo la Magomeni kota.

Akizungumza katika uzinduzi wa nyumba za Shirika la Nyumba NHC jijini Dar es salaam Mkuu wa wilaya kinondoni Sadi Amani amesema kuwa ni vyema wakaazi wanaozunguka mradi huo nivyema wakadumisha hali ya usafi ilikuya wezesha majengo hayo.

"Mheshimiwa Waziri Nina wakumbusha wananchi wanaoishi maeneo haya hapaMagomeni kota kuzingatia Hali ya usafi ilikudumisha ubora wa Majengo haya".Alisema sadi Amani.

Mradi huo unagharimu shilingi billion 10.9 mradi huo watalamu 26 na vibarua 80 nakuwawezesha kutoa mafunzo ya vitendo.

Aidha Said Amani alisema kuwa mradi huo ameiomba serikali kuiongeza bajeti ya miradi ya nyumba za makazi katika maeneombalimbali jijini Dar es salaam.

Naye Mwenyeketi wa kamati ya miundombinu ya Bunge Sulemani Kakoso amesema kuwa Bajeti ya miundombinu ndio bajeti kubwa katika kutekeleza miradi ya nyumba za watumishi.

Alisema wakala wa majengo imekuwa ikiimarika kwa kutumia fedha za bajeti vizuri,amewataka kufanya maboresho makubwa.

"Mheshimiwa waziri muendelee kuipa TBA fedha ilikuhakikisha waweze kuendeleza mingineyo."Alisema Sulemani Kakoso.

Kakoso alisisitiza kuwa nivyema wananchi kuzitunza nyumba hizo.

0/Post a Comment/Comments