WATANZANIA WATAKIWA KUZIPA CHAPUO FILAMU ZA KWAO

*************
 Timothy Marko 

Wito umetolewa kwa watanzania kujenga utamaduni wa kuangalia filamu zinazo zalishwa na wasanii wa filamu hapanchini iliwaweze kuzikosoa iliziweze kuwa na ubora utakao kidhi soko la kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla yautambulisho wa filamu The Green Tanzanite   Mkurugenzi wa bodi hiyo Emmanuel Ndumukwa amesema kuwa nimuhimu kwa watanzania kuzipa kipaumbele filamu zinazo zalishwa hapa nchini ili waweze kutoa tathmini ya ubora wa filamu hizo.

" Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakizipa kipaumbele sana filamu  za nje ,ifike wakati watanzania wakuze utamaduni wa kuziangalia filamu zao ili waweze kuzikosoa ".Alisema Emmanuel Ndumukwa. 

Mkurugenzi Ndumukwa amesema kuwa kwa kujenga utamaduni wa kuziangalia filamu za kitanzania kutachochea wasanii wa filamu kutungeneza filamu bora zenye viwango vya kimataifa. 

Alisema kumekuwa na utamaduni wakuziangalia filamu za nje ya Tanzania  huku wadau wafilamu zakitanzania kulalamikia ubora wa filamu katika viwango vya kimataifa. 

"Watu wengi wamekuwa wakilalamikia ubora wafilamu za kitanzania hali inayochangia soko la filamu  kutokuwa hapa nchini ".Aliongeza Mkurugenzi wa bodi ya filamu Emmanuel Ndumukwa. 

Kwa upande wake  Mzalishaji wa filamu ya kitanzania ya  The Green Tanzanite  Salma Bhamra amesema kuwa Baadhi ya wasanii  wa  kitanzania katika sekta ya filamu wamekuwa wakifanya vizuri katika sekta yauongozaji filamu lakini wamekuwa wakikosa hamasa jambo linalowakatisha tamaa.

Alisema katika nchi za Afrika kusini na Nigeria wamekuwa wakipata hamasa kutoka kwa washabiki na hata pia serikali zao .

Kwa upande wake Mwakilishi wa century cinema shahzaib jafar amesema kuwa filamu nyingi za kitanzania ninzuri lakini zimekosa watu wamasoko katika kuzihamasisha .

"Tunawahamasisha watanzania kujenga utamaduni wa kwenda kuziangalia filamu zao century cinema ".Aliongeza shahzaib Jaffer.

0/Post a Comment/Comments