Mkuu mpya wa wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale,alipo wasili ukumbini na kusalimiana na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Martha Mkupasi.Wageni waakikwa wakishuhudia matukio mbalimbali kwenye hafra hiyo.
WAKAZI wa wilaya ya Chato mkoani Geita,wamemtaka Mkuu mpya wa wilaya hiyo Deusdedith Katwale, kuhakikisha anayasimamia vyema mambo yote yaliyoahidiwa kukamilishwa na rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwenye wilaya hiyo kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.
Ahadi ya rais Samia inatokana na mipango thabiti ya maendeleo iliyotarajiwa kutekelezwa na aliyekuwa rais wa Tanzania,Hayati Dk. John Pombe Magufuli, ambapo rais Dk. Samia Suluhu aliahidi kuyaendeleza ili kuhakikisha ndoto za mtangulizi wake zinatimizwa pasipo vikwazo vyovyote.
Walikuwa kwenye hafra maalumu ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Chato,Martha Mkupasi, ambaye amestaafu utumishi wa umma kisha kumkaribisha mkuu mpya wa wilaya hiyo Deusdedith Katwale.
Mbali na kumpongeza kwa kuteuliwa kwake,wamemtaka kuhakikisha anasimamia vyema miradi yote ya maendeleo na kubuni mipya ili wananchi waweze kunufaika na raslimali za taifa sambamba na kuzitumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao.
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Chato,Mange Ludomya, wananchi wa wilaya hiyo wanayo imani kubwa na uongozi wa Katwale kwa kuwa ni mzaliwa wa wilaya hiyo na mwenye maono makubwa ya kimaendeleo na kwamba wapo tayali kumpa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anatimiza ndoto zake.
Mzee Samweli Bigambo,ametumia fursa hiyo kumpongeza sana aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo (Mkupasi) kabla ya kustaafu, huku akimtakia maisha mema ya ustaafu na yenye mafanikio tele,na kwamba iwapo rais akimhitaji tena asisite kwenda kutumika sehemu yoyote.
Akitoa salaamu zake kwa wajumbe waliohudhuria hafra hiyo iliyoandaliwa na wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa Umma,Mkupasi amedai hakutarajia kupokea pongezi nyingi namna hiyo na kwamba tendo hilo limemtia moyo mkuu,huku akiomba radhi iwapo kuna mtu aliyemkwaza wakati wa uongozi wake.
"Ndugu zangu mimi ni binadamu ninayo mazuri yangu na ninayo mapungufu yangu...naomba kama kuna niliyemkwaza kutokana na uongozi wangu anisamehe sana,maana halikuwa lengo langu kumuumiza mtu badala yake niombe mchuku mazuri yangu ili tusonge mbele"amesema Mkupasi
Kwa upande wake,mkuu mpya wa wilaya hiyo(Katwale) pamoja na mambo mengine amewahakikishia wananchi kuwa ameletwa Chato kufanya kazi na kuwaomba wananchi wampime kwa utendaji wake wa kazi badala ya kutanguliza lawama za kutowatembelea majumbani mwao kwaajili ya salaam.
"Namshukuru sana rais Samia kunileta hapa nyumbani kuwatumikia ninyi...mimi ni mtumishi wenu nipo tayali kuhakikisha nasimamia vyema maendeleo yote yanayoyarajiwa kuwaletea maendeleo wananchi...kikubwa sana naombeni ushirikiano wenu na milango ya ofisi yangu ipo wazi kwa mwananchi yeyote afike tushauriane ili kuijenga wilaya yetu"amesema Katwale.
Mwisho.




Post a Comment