COSTECH KUENDELEA KUUNGA MKONO WABUNIFU NCHINI KUPITIA KONGAMANO LA MWEZI JUNI

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu akizungumzia na waandishi wa habari  akitoa taarifa ya kuelekea kufanyika kwa Kongamano la Kitaifa na maonyesho ya Sayansi na Ubunifu linalotarajiwa kufanyika Juni 14-16 mwaka huu jijini Dar es salaam.

.......................

NA MUSSA KHALID 

Tume ya Sayansi na Teknolojia -COSTECH imesema itaendelea kuwaunga mkono vijana wabunifu ili waweze kunufaika na bunifu mbalimbali wanazozifanya.

 Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt Amos Nungu ametoa kauli hiyo leo  jijini Dar es salaam wakati akizungumzia na waandishi wa habari akitoa taarifa ya kuelekea kufanyika kwa Kongamano la Kitaifa na maonyesho ya Sayansi na Ubunifu linalotarajiwa kufanyika Juni 14-16 mwaka huu.

Dkt Nungu amesema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kuwawezesha watafiti,wabunifu,wanasayansi na wanasayansi kukutana pamoja ili kujadili na kubadilishana mawazo na kupeana taarifa za masuala ya teknolojia na ubunifu nchini.

Aidha amesema kuwa Kongamano hilo ni mkakati wa Tume katika kutekeleza jukumu lake kwa kuwahabarisha watanzania kuhusiana na kazi zinazoendelea nchini na mashirikiano yaliyopo kwa watafiti wandani na nje ya nchi.

Dkt Nungu amesema kuwa kongamano hilo kutakuwa na mijadala mbalimbali sambamba na kuonyesha bunifu ambazo zimefanywa na wabunifu kutoka maeneo mbalimbali.

‘Niseme tu tumeangazia mambo mbalimbali katika Kongamano hilo ikiwemo kuishauri serikali na vyombo vyake kupitia matokeo ya kitafiti zinazofanywa kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu lakini pia watafiti na wabunifu kupata fursa ya kusikiliza kutoka kwa wafanya maamuzi na watunga sera kuhusu mipango ambayo watafiti na wavumbuzi waweze kuifata miongozo hiyo’amesema Dkt Nungu

Kuhusu Mafaniko ya COSTECH Dkt Nungu amesema kuwa Tanzania imekuwa ikinufaika kupitia miradi ambyao inafanywa na wabunifu na hivyo kuunganisha katika mataifa mengine.

Pia Dkt Nungu amemuomba Waziri wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kumualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kushiriki kwenye Kongamano hilo ambalo litakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘Sayansi pamoja na ubunfu kwa maendeleo endelevu’.

0/Post a Comment/Comments