Mfanyabiashara wa huduma za kifedha Mganza,Yohana Mzigaba,akizungumza na mwandishi wetu.
Mfanyabiashara mjini chato,Manyama Kinyonga,akizungumza na mwandishi wetu.
Wadau wa benk ya CRDB wilaya ya Chato,wakiendelea kusikiliza maelekezo kutoka kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo,Deo Mambo.Na Daniel Limbe,Chato
JAMII imeaswa kuachana na imani potofu kuwa wanaochukua mikopo kwenye benki za kifedha nchini kuwa wameishiwa, badala yake watambue ndiyo njia pekee ya kumwinua mwananchi kiuchumi.
Ni kutokana na baadhi ya watu kuwa na sifa za kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha na kushindwa kuitumia fursa hiyo kutokana na kuona aibu ya kuchekwa kuwa hawana pesa za kutosha bila kupata msaada wa benk.
Meneja mahusiano CRDB kanda ya Magharibi,Deo Mambo,amesema hayo leo aprili 27 wakati akizungumza na wadau wa maendeleo wa benk hiyo wilayani Chato mkoani Geita, wakati akiwajengea uwezo wa namna bora ya kuendeleza biashara zao ikiwa ni sambamba na kuwaonyesha fursa nyingi za kiuchumi zanazopatikana kupitia benk ya Crdb.
"Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiona aibu kukopa pesa benk wakiamini watachekwa kuwa hawana pesa au wameishiwa...badala yake wanakwenda kukopa kwa watu binafsi na kutozwa riba kubwa zaidi...jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa mwananchi"
Kukopa siyo dhambi wala haimaanishi kuwa huna pesa...ispokuwa kufanya biashara na benk kunamsaidia mfanyabiashara kukua kwa haraka zaidi ukilinganisha na wasiokopa fedha kwenye mabenk" amesema.
Mbali na mikopo,amesema wananchi wanaweza kutumia benk kuhifadhi fedha zao kwa usalama mkubwa zaidi, kuliko kukaa na fedha nyingi kwenye mito ya vitanda vyao jambo linaloweza kuhatarisha maisha na fedha zao.
Awali Meneja wa CRDB tawi la Chato,Daniel Nyamivugwa, akifungua kikao hicho amewataka wadau hao kutoa ushauri wa namna bora ya kuboresha huduma za benk hiyo ili kama kuna changamoto za kiutendaji ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka ili kuendelea kujenga uhusiano mzuri kati ya benk hiyo na wateja wake.
Kwa upande wake,Yohana Mzigaba,mfanyabiashara wa huduma za kifedha Mganza pamoja na Manyama Kinyonga,wamesema kikao hicho kimewaongezea uelewa mpana wa namna bora ya kutunza fedha zao benk kuliko kutembea na kiwango kikubwa cha fedha mifukoni mwao.
"Kuhusu suala la kukopa fedha benk binafsi naliona ni jambo la msingi sana hasa kwa sisi vijana...ukiogopa kukopa hela benk ujue unanafasi ndogo sana ya kutoboa...mie niwasihi vijana wenzangu tuzitumie fursa hizi za Crdb kujikwamua ki uchumi kuliko kuogopa kufanya kazi wakati fursa zipo za kutosha kupitia benk" amesema Kinyonga.
Mwisho.




Post a Comment