Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia –COSTECH Dkt Amos Nungu wakati akifanya mahojiano
maalumu kupitia Mkutano wake na Vyombo
vya Habari katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma
.........................
Ameyasema
hayo wakati akifanya mahojiano maalumu kupitia Mkutano wake na Vyombo vya Habari
katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma
"
COSTECH mwaka huu tumeleta wabunifu ambao tumekuwa tukiwafadhili kupitia
mashindano ya Kitaifa ya MAKISATU kwa miaka minne (4) ya nyuma tangu mwaka
2019, ambao bidhaa zao tayari zimeingia sokoni " alisema Dr Nungu
Dkt.
Nungu aliongeza kuwa ni muhimu kwa wadau wengine ambao hawakupata nafasi ya
kufikiwa na COSTECH kutumia Jukwaa la Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa
(Innovation Week) inayoendelea kuadhimishwa kuanzia tarehe 24 - 28 Aprili 2023
ili kutangaza bunifu zao kwa watanzania.
"
Pia nitoe wito kwa wananchi, wadau wa maendeleo na sekta binafsi kuja kujionea
na kuwekeza katika hizi bunifu, kuona
kwenye kuendeleza ubunifu
"
Vilevile tunayo Taasisi inayofanana na COSTECH toka Afrika kusini ambao
tunakutana mara kwa mara kujifunza na kuna wakati tulishafadhili bunifu
nyingine pamoja, nao pia wamekuja kushiriki ili kuipa hadhi Wiki ya Ubunifu
kuongeza Sura ya Kimataifa " alisisitiza Dkt. Nungu
Alihitmisha kuwa Mwezi wa sita (6) COSTECH inategemea kuwa na Kongamano la Ubunifu maarufu kama STICE katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kituo cha Mwalimu Nyerere - JNICC, jijini Dar es Salaam.


Post a Comment