MCHECHU ATOA WITO KWA TAASISI ZA UMMA KUWA NA BODI IMARA






 .,....................

Timothy Marko .

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu amezitaka Mashirika ya umma pamoja na taasisi binafsi kuwa na bodi imara ili iweze kujiendesha kibiashara.

Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha Wakurugenzi wa taasisi za serikali na binafsi jijini Dar es salaam Nehemia Mchechu amesema kuwa nivyema taasisi za umma na binafsi kuwa na bodi imara katika kuendesha taasisi hizo ilikuwepo na tija katika taasisi zao.

 "Lazima taasisi ziwe nabodi zitakazowezesha taasisi hizo kujiendesha Kibiashara ".Alisema Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu. 

Mchechu alisema kuwa nivyema taasisi za ummazioneshe waziwazi katika mchango wa kujenga uchumi nakukuza pato la taifa.

Aliongeza nivyema taasisi hizo ziweze kuonesha mchango katika ukuaji katika sekta ya ajira nchini.

"Nivyema Mashirika haya ya umma yaoneshe yamechangia vipi katika sekta ya ajira "Alisisitiza Mchechu.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Anga nchini Hamza johari amesema kuwa nivyema uboreshaji wa Mashirika ya umma yaendesambamba na kuboresha mipango mikakati yatakayo boresha Mashirika hayo ya umma. 

"Katika mabadiliko haya yaendane sambamba na uboreshaji wa mifumo ya kitaasisi".Alisema Hamza Johari.

0/Post a Comment/Comments