Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii
-Nct, Bi Jesca William Akizungumza Jijini Dar Es SalaamWadau
wa waratibu matukio -MC's, wakifatilia mafunzo ya Chuo cha Taifa cha Utalii
Na: Issa Mohamed.
Email: issahmohamedtz@gmail.com
Kaimu Makamu Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Utalii –NCT, Bi Jesca William amesema chuo hicho
kimekusudia kuwatumia waratibu matukio –MC ili kujipambanua katika kutangaza
sekta ya Utalii kupitia kumbi mbalimbali za mikutano.
Ametoa Kauli hiyo
Jijini Dar es salaam katika mafunzo ya Muda mfupi na kuwakutanisha wadau wa
tasnia hiyo lengo ni kuwatambulisha fursa mbalimbali zinazotolewa na Chuo
hicho.
Amesema ni wazi kuwa
tasnia hiyo imeendelea kukua kwa kasi ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaelekeza
wadau wanaoratibu matukio kujikita zaidi katika kutangaza utalii wa matukio ili
kukuza pato la Taifa kupitia sekta hiyo.
‘’Kwa sasa hivi
tunaangalia kama chuo tunaweza kusaidia uratibu wa mikutano ili kukuza Utalii
lengo letu ni kutaka kuangalia mahitaji alisi ya soko pamoja na kuleta program
mbalimbali ili kuwa chachu ya kukuza utalii hapa Nchini’’ Amesema Bi Jesca
Nao baadhi ya wadau
walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa watatumia nafasi hiyo kutangaza Utalii
huo hasa wakati wa kusherehesha matukio katika kumbi mbalimbali.
Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii imeonesha kuwa sekta hiyo huchangia asilimia 25 ya fedha za kigeni na zaidi ya asilimia katika pato la Taifa –GDP.


Post a Comment