NMCP KUTOKOMEZA MARALIA IFIKAPO 2030


********

Timothy Marko 

Taasisi ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP)imesema hali ya ueneaji wa ugonjwa wa Maralia imepungua kutoka Asilimia55 hadi kufikia Asilimia53 wakati huo huo vifo vinavyotokana na ugonjwa huo vimepungua kutoka 6,311 kwa mwaka 2015 hadi kufikia 1,502kwa kipindi cha mwaka jana.

Akizungumza katika kongamano la kutathimini hali ya Maralia nchini jijini Dar es salaam Mkuuwa kitengocha vipimo na Matibabu wa taasisi ya udhibiti hali ya Maralia Dk.Abdallah Lusas amesema kuwa mikoa inayoongoza kuenea kwa ugonjwa huo Tabora pamoja na mkoani Mara .

"Hali ya Maralia imeshuka kwa asilimia 41wapo Chini ya Maambukizi ".Alisema Dk Abdalah Lusasi.

DK Lusasi alisema kuwa ueneaji wa ugonjwa wa maralia umegawnyika kikanda kanda ya Magharibi Tabora wakati kanda yakusini nipamoja na Mtwara ambapo hali yamaralia ipo juu.

"Mikoa ambayo ipo katika halinzuri ya udhibiti wa maambukizi ya Maralia nipamoja na Tanga nakilimanjaro".aliongeza Dk Lusasi. 

Dk lusasi aliongeza kuwa vifovingi vya ugonjwa Maralia huwapata hasa watoto ambapo Jumla ya Halimashauri 56 zimebainika kuwa kiwango chajuu cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Maralia. 

"Kampeni ya matumizi ya afua za dawa zimesaidia kupunguza hali ya Maralia ".alisisitiza Lusasi. 

Katika hatua nyingine Lusasi alisemakuwa tasisi hiyo imelenga kutokomeza ugonjwa huo kufikia Maambukizi 0 ifikapo Mwaka 2030.

0/Post a Comment/Comments