Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Prof. Carolyne I. Nombo ameyasema hayo, leo tarehe 28 Aprili 2023 wakati wa Hafla ya kuhitimisha Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa (Innovation Week) iliyodumu kwa Siku tano (5) kuanzia tarehe 24 - 28 Aprili 2023, Uwanja wa Jamhuri - Jijini Dodoma
" Maadhimisho yanatoa fursa kwa wabunifu kuingiza bidhaa za kibunifu na Teknolojia mpya sokoni baada ya kuendelezwa na Serikali ili ziweze kutumika na jamii ya Watanzania, Mpaka sasa bunifu 53 zimefikia hatua ya kubiasharishwa na kuanza kutumika sekta ya kilimo " alisisitiza alisema Prof. Nombo
Vilevile, Prof. Nombo amefafanua kuwa Serikali imepokea wabunifu toka Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Taifa la Afrika kusini na ujumbe toka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADEC.
" Serikali inayoongozwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua changamoto za wabunifu na iliwezesha ujenzi wa kumbi bunifu ya BUNI HUB na Atamizi ya DTBI zinazosimamiwa na COSTECH , imefanikiwa kuzalisha makampuni machanga 94 yanayochangia pato la Taifa kwa kodi zaidi ya TZS Millioni 500 pamoja na kutoa fursa za ajira kwa wastani wa watu watano (5) hadi thelathini (30) nchini " alisisitiza
Aidha, Aliongeza Makampuni hayo yamejikita kwenye Sekta ya Tehama, Kilimo na Bioteknolojia ikijumuisha kampuni ya Magilla Tech, Guavay biotechnology Co ltd, Agri Info , Time Ticket na Sahara Ventures zilizopitia kumbi ya BUNI HUB na Atamizi ya DTBI chini ya usimamizi wa COSTECH kabla ya kujitegemea na kuwa makampuni za kibiashara na mchango wake unatambuliwa na Serikali" aliongeza Prof Nombo
Ili kuhakikisha programu, kumbi bunifu na Vituo vya atamizi vinaongezeka kwa wingi nchini, Serikali imeendelea kulea na kuzalisha bunifu mpya kupitia Wizara ya Elimu na COSTECH kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa kumbi bunifu na vituo vya atamizi vipya vya atamizi katika Vyuo Vikuu
" Wizara inatoa hamasa ya ushiriki toka wadau wa maendeleo kwa lengo la kuongeza maarifa ya wahitimu wa elimu Vyuo vya elimu ya juu na ya kati kupitia kumbi bunifu kama vile UDSM , SUA , UDOM, MUST pamoja na atamizi ya Zanzibar Technology & Business Incubators - ZTBI "


Post a Comment