MWEKEZAJI MIRERANI AJITOSA KUMFAGILIA RAIS SAMIA

 




****************

Na Richard Mrusha Manyara 

MMILIKI wa Kampuni ya Ngabomoa,iliyopo Mirerani mkoani Manyara,ameonyesha kufurahishwa na juhudi za rais Samia Suluhu Hassan, kuvutia uwekezaji nchini kupitia filamu ya "Royal tour" huku akiahidi kuwekeza zaidi.

Kampuni hiyo,inamiliki Hotel za kitalii ikiwemo, Ngabomoa,Tembo raha na Montel lodge zote zikiwa katika wilaya ya Simanjiro ambapo baadhi ya wageni wa ndani na nje ya nchi wamekuwa wakivutiwa nazo.

Akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea baadhi ya hotel hizo kwa lengo la kujionea fursa za uwekezaji huo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Gaspal Ngabomoa Swai, ametumia fursa hiyo kumpongeza rais Samia Suluhu kwa kuhamasisha uwekezaji nchini jambo ambalo limeanza kuzaa matunda kwa ongezeko la watalii.

Mbali na pongezi hizo amesema kuelekea sikukuu za Pasaka na Id –El Fitir, anatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa Kilabu ya kisasa kwa lengo la kuongeza burudani kwa wateja wao.

“Kwakweli katika maisha yangu nilipitia changamoto kubwa sana na ndio maana nikaamua kufanya uwekezaji huu hususani hapa Mirerani...kimsingi niliamua kujiajiri mimi mwenyewe na pia niweze kuajiri watanzani wezangu na nimetoa fursa ya ajira kwa watanzania wezangu...kadri inavyokwenda nitaendelea kuajiri watanzania zaidi na hapa namshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa moyo wake wa upendo kwa kutujali wawekezaji wazazwa" amesema Ngabomoa.

Amesema miaka miwili ya rais Samia Suluhu akiwa madarakani baada ya kupokea kijiti kutoka kwa aliyekuwa rais wa Tanzania,Dk. John Pambe Magufuli, ameweza kurudisha hali ya mshikamano na amani ndani na nje ya nchi na kwamba amekuwa mtetezi wa wafanyabiashara,jambo linalowapa ujasiri wa kumuunga mkono jitihada zake.

Kwa upande upande wake Meneja wa Hotel hiyo, Dismas Deus Kagandiga na msaidizi wake Halima Hamza wamesema matarajio yao ni kuendelea kuboresha huduma zao ili kuwavutia wageni kutembelea wilaya ya Simanjiro na kuhamasisha uwekezaji mkubwa jambo litakalo punguza uhaba wa ajira kwa vijana.

                     Mwisho.

0/Post a Comment/Comments