Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la uwakala wa Meli Nchini -TASAC Kaimu Mkeyenge akizungumza katika
mkutano uliolenga kutoa uelewa katika shughuli za utafutaji na uokoaji Jijini
Dar es salaam
....................
Na: Issa Mohamed –Dar
es salaam.
Email: issahmohamedtz@gmail.com
Naibu Katibu Mkuu
wizara ya ujenzi na uchukuzi anayesimamia sekta ya uchukuzi Dkt Ally Possi
amesema kuna haja ya wataalamu wa sekta ya Bahari Nchini kupendekeza changamoto
zinazoikumbuka sekta hiyo hasa katika swala zima la uokoaji pale ambapo majanga
yanapotokea.
Dkt Possi ametoa kauli
hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tano
yaliyowakutanisha shirika la uwakala wa meli Nchini –TASAC kwa kushirikiana na
Shirika la Bahari Duniani –IMO lengo ni kutoa uelewa katika shughuli za
utafutaji na uokoaji.
Amesema hatua stahiki
za uokoaji zisipochukuliwa Taifa litapunguza kuaminiwa pamoja na kuhatarisha
sekta nyingine ikiwemo usafirisha pamoja na sekta ya Utalii.
‘’Lazima tutambue
Taifa letu linakabiliwa na changamoto gani kwahiyo wadau hawa watumie mkutano
huu wa siku tano kuleta mapendekezo kwa serikali na sisi tutazichuku na
kuzifanyia kazi’’ Amesema Dkt Possi
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la uwakala wa meli Nchini –TASAC Kaimu Mkeyenge
amesema tayari serikali imeanza kutekeleza mkataba wa uanachama wa shirika la
Bahari Duniani hasa katika kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya Bahari.
‘’Kimsingi Nchi ya
wanachama wa shirika hili la Bahari Duniani wanapaswa kutekeleza mkataba huu na
sisi kama Tanzania tayari tumeshauridhia na hatuna budi kutekeleza mkatana
ule’’ Amebainisha Mkeyenge.
Nao baadhi ya
washiriki wa mkutano huo wamesema kuwa mafunzo hayo yawatasaidia katika
kusimamia shughuli za utafutaji na uokoaji hatua ambayo itapunguza vifo
vitonavyo na majanga hayo.
Mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari Duniani umeanza kutekelezwa tangu mwaka 1985 ambapo Tanzania ni miongoni mwa Nchi ya wanachama wa mkataba huo.
Post a Comment