SERIKALI YAITAKA TRA KUSHIRIKIANA NA WACHIMBAJI WADOGOWADO KATIKA MIPANGO YA KIKODI.




*************


Timothy Marko. 

SERIKALI imewataka Mamlaka, ya  Mapato nchini (TRA)kutoa taarifa ya,mipango ya kimkakati ya kikodi ili  wawachimbaji wadogo wadogo wamadini nchini kuwasadi wachimbaji wadogowado kuweza kulipa kodi pasipipokuwa na vikwazo vyoyote.

Akizungumza katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa madini wa sekta hiyo ya madini ya Viwandani         waziri wa madini Doto Biteko amesema dhima kuu ya serikali kupitia sekta hiyo nikuhakikisha wachimbaji wadogowadogo wa madini ya viwandani Mazingira yao yanaboreshwa.

"Ningetamani wachimbaji wakubwa na wadau wa sekta ya madini ya viwanda wanawapa nafasi wachimbaji wadogowadogo  ili waweze kukua ".alisema Waziri wa Madini Dotto Biteko.

Waziri Biteko aliwataka wadau wasekta ya viwanda kushirikiana na wachimbaji wadogowadogo katika upangaji wa bei ya madini.

Alisema kuwa sekta ya madini imekuwa ikileta mchango mkubwa katika kukuza ajira nakodi sambamba nakukuza uchumi.

"Lengo la serikali nikuhakikisha sekta ya madini inamarika hasa madini ya viwandani."Aliongeza Waziri Dotto Biteko. 

Naye Mwenyeketi wa Chama cha wachimbaji Madini Mkoa wa Dar es salaam Joseph at Mkombachepa amesema kuwa sekta hiyo imekuwa ukikua kwa kasi nakuchangia pato la taifa kwa asilimia 10.

0/Post a Comment/Comments