"""""""""""""""""
Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewapongeza wana Dodoma kwa kuanza shamrashamra za kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar ikiwa ni wiki ya maadhimisho sherehe hiyo na kuwataka vijana kuchangamkia fursa zinazoendelea kujitokeza jijini Dodoma.
Senyamule ameyasema hayo leo alipotembea eneo la mradi wa ujenzi wa uwanja na mnara wa mashujaa katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba.
‘’Leo nina furaha kubwa kwa kuwa maelekezo ya Mhe Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapa jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa yanaendea kutekelezwa na hii ni heshma kubwa kwetu wana Dodoma kwakuwa Mradi huu unaanza kutekelezwa kwa vitendo. Kupitia mradi huu, tunakwenda kuweka alama nyingine muhimu itakayopendezesha Mkoa wetu ambao ndio Makao Makuu ya Nchi yetu, pia wanadodoma watanufaika kiuchumi na kijamii” Senyamule amefafanua
Aidha Mhe. Senyamule amewataka wakandarasi kuhakikisha wanatekeleza ujenzi wa mradi kwa hadhi kubwa na sifa nzuri kwa kuzingatia ubora na imara kwa miundombinu na kuzingatia muda waliopatiwa.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amezungumzia maandalizi ya Mkoa wake kuelekea maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano.
"Tunaelekea kusherehe ya miaka 59 ya Muungano wetu tarehe 26/4/2023 na hapa Dodoma tumeanza kuadhimisha toka tarehe 17/4/2023 ambapo tunajivunia mashujaa wetu walioweza kuunganisha Tanganyika na Zanzibar na kuleta Tanzania ambayo hii leo tunajivunia Muungano wenye mshikamano ,usio yumba, wenye mtizamo sahihi kwa wananchi wake wa pande zote mbili na muungano ulio imarika kila sekta kwa Tanzania na Dunia kwa ujumla "Amesema Senyamule
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Jimmy Yonaz amesema fedha za ujenzi zipo na zinatoka kwa wakati ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 17 zitatumika kufanikisha ujenzi wa Mnara huo wa mashujaa pamoja na miundombinu mingine katika eneo hilo na kusisitiza kuwa upande wa usimamizi wamejipanga ipasavyo.
Ujenzi wa mnara huo unanajengwa na kampuni ya SUMA JKT



Post a Comment