STAMICO, CTI NA DACOREMA KUKUTANA NA WACHIMBA WADOGO APRIL 05 HADI 06.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa -STAMICO, Dkt Venance Mwasse akizungumza na waandishi wahabari kuelekea mkutano wa wachimbaji wadogo wa Madini kesho April 05.Mwenyekiti wa wa shirikisho la wenye Viwanda Nchini -CTI, Leodigar Tenga akizungumza na waandishi wahabari kuelekea mkutano wa wachimbaji wadogo wa Madini kesho April 05

Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini -DACOREMA, Josephat Mkombachepa
................

NA: Issa Mohamed.

EMAIL: issahmohamedtz@gmail.com

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa –STAMICO, Dkt Venance Mwasse amesema serikali imekusudia kukutana na wachimbaji wadogo wa madini wa viwandani pamoja na wenye viwanda ili kujadili changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Ametoa  kauli hiyo Jijini Dar es salaam katika kuelekea mkuano wa wachimbaji wadogo na wadau wa madini wa viwandani ulioshirikisha taasisi mbalimbali ikiwemo –STAMICO, Shirikisho la wenye viwanda –CTI, pamoja na chama cha wachimbaji madini mkoa wa Dar es salaam na Pwani –DACOREMA.

Amesema serikali imekusudia kuvuna rasilimali za madini kwa maslahi mapana ya Taifa hivyo mkutano huo umelenga kutambua changamoto kutoka kwa wadau hao pamoja na kuwa na mkakati wa pamoja kuhusu sekta ya madini.

‘’Mungu ametubariki kuwa na rasilimali za madini kila mahali sasa tunataka zinavunwa kwa tija ili kuwa chanzo cha kuendeleza maendeleo ya Nchi hivyo natoa wito kwa wachimbaji wa wadogo wa madini kuchangamkia fursa hii’’ Amesema Dkt Mwasse.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la wenye viwanda Nchini –CTI, Leodigar Tenga amesema ili uchumi uhimarike ni lazima wadau husika washirikishwe ikiwemo kusikiliza maoni yao.

‘’Tuna madini yetu Nchini sisi kama –CTI tunahamasisha wanachama wetu kujikoteza kwa wingi ikiwemo kuingia katika ushindani hasa katika soko la Madini’’ Amebainisha

Naye Mwenyekiti chama cha wachimbaji wadogo wa Madini –DACOREMA, Josephat Mkombachepa amesema Tanzania lazima iwe kisiwa cha soko la madini endapo changamoto mbalimbali zitatatuliwa.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza April 5 hadi 6 mwaka huu huku Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana ya Madini Dkt Dotto Biteko na umebebwa na kauli isemayo ‘’Madini ya Viwandani kwa uchumi wetu na mazingira bora’’

0/Post a Comment/Comments