Timothy Marko
Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini (LATRA)imewataka wasafirishaji ikiwemo Dalala kuboresha huduma ikiwemo kuhimiza matumizi ya utoaji wa tiketi kwa njia ya kieletroniki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Habib Suluo amesema kuwa sambamba nakuhimiza tiketi za kieletroniki pia Mamlaka ya Latra imebaini mapungufu kwa watoa huduma ya ufuatialiaji Mwenendo (VTS) mamlaka hiyo imewasimamisha watoahuduma wa vifaa vya udhibiti mwendo wa mabasi ambapo vifaa hivyo vimebanika kuchezewa na baadhiya makakapuni.
" Makampuni ambayo yamebanika kakichezea mifumo ya VTS ambapo makakapuni haya yametakiwa kurekebisha kasorozlizobainika kwenye mabasi yalifungiwa na wakikamisha watarudishwa kuendelea na utoji wa huduma ya kufunga vifaavipya". Alisema Mkurugenzi Habibu sululo.
Mkurugenzi sululo alisema kuwa kutokana na hitiliafu ya mfumo wa VTS mamlaka imebaini kuwa vifaa vyake vimeharibiwana mifumo ya umeme kuharibiwa
Alisema kuwa kuna baadhi ya magari yamebadili mifumo ikiwemo switch ya kuzima na kuwasha .
"Kibaya zaidi mifumo ya software imekuwa ikituma taarifa za uongo kwenye mfumo ya ufuatiliaji".Aliongeza Habib Suluo .
Sululo alisisitiza kutokana kasorohizo kikosi cha usalama barabarani imewasimamisha madereva 15 kutokana na kuharibu mifumo ya VTS.


Post a Comment