WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAENDELEA KUTANGAZA UTALII, YAINYUKA TCDC MASHINDANO YA MEI MOSI*




                             **************
Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kuutangaza utalii kupitia michezo ya Mei Mosi Kitaifa 2023 inayoendelea mkoani Morogoro.

Akiongea baada ya michezo iliyofanyika  leo April 20, 2023, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu kutoka Wizara hiyo Bi Prisca Lwangili amesema wataendelea kutumia fursa hiyo kuutangaza utalii kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya “The Royal Tour” 

“ Timu yetu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii imecheza mchezo mzuri sana. Ni mabingwa watetezi wa kombe la Mei Mosi na tunapania kuhakikisha kuendelea kuwa mabingwa tena kwa mwaka huu " 

Kwa upande wa Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu Carlos Mbilo amesema wanatumia michezo hiyo kama fursa ya kuutangaza utalii.

Katika mchuano wa  leo Wizara ya Maliasili na Utalii  imechezwa michezo miwili ya  kwa upande wa mpira wa miguu dhidi ya Tanesco zimetoka  suluhu ya bila kufungana na pia mpira wa wavu dhidi ya Ushirika (TCDC) imeibuka  kidedea kwa kuifunga Timu hiyo seti mbili kwa sifuri.

0/Post a Comment/Comments