Timothy Marko
CHAMA cha ACT wazalendo kimeitaka Serikali kuimarisha mifumo ya kikodi katika usimamizi wa sekta yakilimo nchini ilikuleta tija katika sekta hiyo.
Aidha Chama hicho kimeiomba serikali kuweka mifumo ya uendeshaji wa sekta ya kilimo ilikuhakikisha wakulima wananufaika na sekta hiyo nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri kivuli wa kilimo wa chama hicho Mtutura Abdalah amesema kuwa sekta yakilimo imekuwa ikitoa ajira Asilimia 65na nguvu kazi ya watanzania wote nakuchagiza upatikanaji wa chakula Asilimia 100.
"Bado hali za wakulima hazijabadilika nakunufaika nakilimo ".Alisema Mtutura.
Mtutura Aliongeza kuwa
kumekuwa na malamiko ya wakulima wa Tumbaku mkoani Tabora bei ya zao hilo limeshuka kwa Asilimia 35 ya soko la dunia.
Aliongeza kuwa nivyema serikali ikawekeza kilimo chaumwagiliaji ilikuondokana njaa.
"Mabonde kama vile ziwa vitoria, Maragalasi,mtoRuvu nimahususi kwakilimo cha umwagiliaji".alisisitiza Mtutura.


Post a Comment