AGA KHAN YAZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUTOA Elimu YA MIKOPO KWA VIJANA

                 *******


Timothy Marko. 

Taasisi za kibiashara zimetakiwa kutoa Elimu ya Biashara kabla yakutoa mikopo kwa vijana ili waweze kujiari .

Akizungumza katika kongamano la uwezeshaji mikopo kwa vijana lililoandaliwa na taasisi ya Aga khan Foundation Meneja Miradi wa taasisi hiyo  Simon  Meigaro amesema kuwa taasisi hiyo imelenga kukuza uwezo wa vijana katika kujiajili. 

"Kumekuwa na tatitizo kwa mikopo mingi ya vijana kutorudi pindi vijana wanapoomba mikopo hii inatokana na kuwepo kwa Elimu duni ya kuanza biashara ".alisema Meneja Miradi wa Agakhan Foundation Simon Meigaro.

Meneja Miradi Meigaro alisema kuwa Mpango wa utoaji wa Elimu ya Biashara utajumuisha mikoa ya Mwanza ,lindi  Dar es Salaam  Mtwara.

Naye Katibu wa Baraza la kuwawezesha Wananchi kiuchumi Bengi Issa amesema kuwa kumekuwa na mwamko mdogo kwa wanawake katika kufanya biashara sambamba na 
matumizi madogo yakufanya biashara mtandaoni hasa kwa wanawake waliopo katika maeneo ya vijijini.

Alisema utaratibu wa kupataz mikopo kwa wanawake kutoka Halmashauri nilazima wanawake hao wakajiunga kikundi kisicho pungua watu watano na kuwa na akiba kwenye Akaunti.

"Kumekuwa na mwamko mdogo katika matumizi ya teknolojia katika kufanya biashara ".Alisema Bengi Issa.

0/Post a Comment/Comments