AICT KUANZA KUSAMBAZA MASAFA YA INLAND FM KWENDA MIKOANI.



*******

Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano AICT Fabian Fanuel leo amefanya ziara ya kikazi katika Dayosisi ya Shinyanga ambapo amepata nafasi ya kufanya mazungumzo ya na Makamu Askofu Mkuu AICT na ambaye ni Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Enock Bugota ofisini kwake.

Katika ziara ambayo imehusisha mambo kadha ya kiutendaji kama vile kujitambulisha baada ya uteuzi wa nafasi hiyo pamoja na majadiliano ya kazi ambazo zinaendelea katika Dayosisi hiyo katika nyanja mbalimbali.

Kadhalika mazungumzo hayo yamejikita katika Maandalizi ya tamasha kubwa la Inland Festival 2023 katika Dayosisi ya Shinyanga na uwashwaji wa matangazo ya Inland Radio katika Mkoa wa Shinyanga.

Vilevile Fanuel amepata muda wa kukaa kikao cha kwanza na kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambalo kwa Dayosisi ya Shinyanga linategemea kufanya maeneo manne tofauti kama vile Bariadi, Maswa, Kahama na Shinyanga Mjini.

Kwa upande Askofu Bugota amepongeza kazi ambazo Idara ya Habari na Mawasiliano AICT imekuwa ikifanya katika kutekeleza majukumu na mikakati yake ya kila na kuiomba iendelee kufanya kazi kwa nguvu kuhakikisha wanafikia malengo tarajiwa.

0/Post a Comment/Comments