Mratibu wa Jukwaa la Asasi za kiraia Zanzibar Dkt. Mahfoudh Shabani Haji akizungumza na waandishi wa habari wakati wa jukwaa la Asasi za kiraia liliundwa na shirika la Kimataifa la uhifadhi wa mazingira WWF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo Jumatano Mei ,03, 2023 katika Ukumbi wa Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam.
Msimamizi wa miradi ya Bara na Pwani kutoka Shirika la WWF Dkt. Modesta Medard akizungumza na waandishi wa habari wakati wa jukwaa la Asasi za kiraia liliundwa na shirika la Kimataifa la uhifadhi wa mazingira WWF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo Jumatano Mei ,03, 2023 katika Ukumbi wa Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzindua Jukwaa la Asasi za kiraia liliundwa na shirika la Kimataifa la uhifadhi wa mazingira WWF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambalo litakwenda kufanya kazi maeneo ya Kanda na Pwani katika kushughulikia masuala ya uchumi wa Bluu, leo Jumatano Mei ,03, 2023 katika Ukumbi wa Hotel ya Protea Jijini Dar es salaam .
**********
Na Mwandishi wetu
Asasi za kiraia na wadau wa maendeleo wamesema wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuweza kufikia malengo ya kuwa uchumi wa bluu endelevu kupitia sera, mikakati pamoja na miongozo mbalimbali.
Hayo yamesemwa jana Jumatano Mei 03,2023 Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Jukwaa la Asasi za kiraia Zanzibar Mahfouz Shabani Haji wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Asasi za kiraia liliundwa na shirika la Kimataifa la uhifadhi wa mazingira WWF kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambalo litakwenda kufanya kazi maeneo ya Kanda na Pwani katika kushughulikia masuala ya uchumi wa Bluu.
Amesema kuwa jukwaa hilo ni mahsusi katika kusaidia kuongeza nguvu zinazofanywa na wadau mbalimbali kukuza uchumi wa bluu endelevu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja kuanzia ngazi ya chini katika jamii za maeneo ya Pwani.
" Tunaamini katika bahari kuna rasilimali nyingi zinazohitaji kusimamiwa kwa kuwajengea uwezo Wananchi na kuwashirikisha ili kuweza kuwainua katika kazi zao wanazozifanya maeneo ya Pwani.
Kwa upande wake Msimamizi wa miradi ya Bara na Pwani kutoka Shirika la WWF Dkt. Modesta Medard amesema jukwaa hilo litaenda kusukuma jitihada za kujenga uchumi wa bluu katika sekta za Pwani na bahari.
Amesema WWF iliona umuhimu wa kuanzisha Jukwaa hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar katika kuandaa sera na miongozo ya kutekeleza suala la uchumi wa bluu.
" Jamii ya Pwani ilikua inaangaliwa kama jamii maskini jambo ambalo si kweli bali tunahitaji kuongeza kasi ya kuwekeza ili tuweze kubadilisha maisha ya jamii ya Pwani" amesema Dkt. Modesta
Naye Mwakilishi wa taasisi ya milele Zanzibar Foundation amesema kuundwa kwa Jukwaa hilo kutaunganisha nguvu za wadau kuweza kufikia lengo la kuwa na uchumi wa bluu endelevu.



Post a Comment