Watanzania ambayo wako kwenye Mikoa yenye kiwango kikubwa cha ugonjwa wa malaria wameshauriwa kutumia dawa za kuulia viwadudu vya mazalia ya mbu ili kuweza kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni mkono juhudi za serikali za kutekeleza mpango mkakati wa kutokomeza maralia.
Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania Nchini CUBA Humphrey Polepole wakati wa Ziara ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha dawa za kuua viwadudu cha Bio Tech kilichoanzishwa Mwaka 2007 kwa kushirikiana na Cuba na Tanzania ikiwa ni sehemu ya kuendeleza mashirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
"Kiwanda hiki cha Bio Tech kimeanzishwa Mwaka 2007 kwa kushirikiana na Cuba na Tanzania ikiwa na lengo la kuteketeza Vijidudu vya Maralia ".Alisema Balozi Humprey Pole pole.
Balozi pole pole amesema takwimu zinaonesha kuwa mikoa Tabora imekuwa Kinarakatika kuzalisha vimelea vya ugonjwa wa Maralia kwa Asilimia 23 wakati Mkoa wa Mtwara unashika nafasi ya pili katika maambukizi na Kagera kwa asilimia 18 huku mkoa Mara ukishika nafasi ya tatu Asilimia15 na kigoma asilimia 13.
Aliongeza kuwa lengo ni kuhakikisha suala la ugonjwa wa Maralia kuwa historia ifikakapo 2025.
"Kule Cuba Hakuna Maralia wala Mbu ,ugonjwa wa Maralia umekuwa ukiongoza kwa Vifo kwa watu wetu".Alisisitiza Balozi Humprey Pole pole.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Cuba Yordenis Despougne alisema kuwa Ushirikiano baina ya Tanzania na Cuba katika kutokomeza ugonjwa wa Maralia ni wakipindi kirefu.
Alisema Nchi yacuba imekuwa na mashirikiano ya muda mrefu katika kupambana na ugonjwa wa Maralia nakukuhakisha ugonjwa huo unakuwa historia hapa nchini.
"Nchi ya Cuba imekuwa mstari wa mbele katika kukukuza ushirikiano na nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania katika kuteketeza Vijidudu vya Maralia kwa kushirikiana na nchi jirani."Aliongeza Yordenis Despougne.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa shirika la maendeleo la Taifa NDC Nicolaus Shombe amesema Takwimu zinaonesha kumekuwa navifo 36 kila mwaka vinatokana ugonjwa wa Maralia ambapo lengo nikuhakikisha vifo hivyo vinatokomea kabisa ifikapo 2025.
Naye Mdhibiti ubora wa ubora Samweli Mzirai Bio Tech amesema Takwimu zinaonesha kumekuwa navifo 36 kila mwaka vinatokana ugonjwa wa Maralia ambapo lengo nikuhakikisha vifo hivyo vinatokomea kabisa ifikapo 2025.

Post a Comment