BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LAMPONGEZA RAIS SAMIA KUONYESHA UKOMAVU KWENYE SIASA

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa Tanzania Juma Ali Khatib akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam akiwaeleza kuhusu maazimio ya Mkutano wa Leo wa wadau wa siasa.
 ....................

NA MUSSA KHALID 

Baraza la Vyama vya Siasa nchini limempongeza Rais Dkt Samia Suluh Hassan kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa na utayari katika suala la upatikanaji wa Katiba mpya.

Hayo yamejiri kufuatia Maagizo ya Rais Dkt Samia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mstaafu Fransis Mutungi kumtaka aitishe baraza likiwahusisha wadau wa siasa ili kujadili upatikanaji wa Katiba Mpya.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa ambayo umeitishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa Tanzania Juma Ali Khatib amesema wanaipongeza hatua hiyo hivyo dhamira yao kufanya utekelezaji.

Aidha Mwenyekiti huyo ameipongeza serikali kwa kutenga bajeti maalum ya Baraza la Vyama vya Siasa kwa Kila mwaka kupatiwa Tsh.Bill 1.5 jambo ambalo litasaidia kukuza demokrasia na kujenga siasa bora na za maridhiano.

‘Baraza hili pia limeazimia kuwa mkutano mkubwa wa wadau utafanyika mwezi wa nane mwaka huu lakini kuanzia mwezi wa sita wajumbe wa baraza wataanza kupatiwa mafunzo maalum na taarifa maalum ya kikosi kazi kwa ajili ya mchakato wa upatinaji wa katiba mpya.’amesema Khatibu

Amesema katika mkutano huo watawashiriki wadau mbalimbali katika kupata maoni wakiwemo taasisi za kidini,asasi za kirai,watu mashuhuri pamoja na baadhi viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima AFP Mack Isdory Mhemela akiwa ni mshiriki wa mkutano amesema wananchi kuendelea kuwaamini ili waweze kufanikisha mipango mbalimbali ya kisiasa wanayoifanya ikiwemo upatikanaji wa Katiba mpya

0/Post a Comment/Comments