Wapili kutoka mbele ni mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akikagua ujenzi wa shule mpya ya Msingi Kaseni iliyopo Kachwamba Chato
Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Kaseni iliyopo Kata ya Kachwamba
Viongozi mbalimbali wakitazama ubora wa majengo ya shule mpya ya msingi Kaseni
Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Kaseni iliyopo Kata ya Kachwamba.
**********
Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Kaseni iliyopo Kata ya Kachwamba
Viongozi mbalimbali wakitazama ubora wa majengo ya shule mpya ya msingi Kaseni
Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Kaseni iliyopo Kata ya Kachwamba.
**********
Na Daniel Limbe,Chato
KATIKA kukabiliana mrundikano wa wanafunzi wa shule za msingi kwenye kata ya Makurugusi na Kachwamba wilayani Chato mkoani Geita,halmashauri ya wilaya hiyo imepongeza kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa shule hizo.
Shule hizo ni mpango mkakati wa serikali wa kupunguza msongamano wa wanafunzi pamoja na kuinua taaluma kwa wananfunzi waliopo wilayani humo.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Marthine Shigela,ametoa pongezi hizo baada ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Kaseni iliyopo kata ya Kachwamba ambayo inatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 400 kukamilika kwake.
Hata hivyo, Shigela amesisitiza uadilifu katika ujenzi na usimamizi wa miradi ya umma,sambamba na kuwalipa kwa wakati wakandarasi na mafundi katika ujenzi huo kutokana na kile alichodai kuwa fedha za miradi hiyo zipo.
"Watu waliamini kuondoka kwa Hayati Magufuli ndiyo ingekuwa mwisho wa maendeleo kwenye wilaya yetu na mkoa wa geita...nataka niwahakikishie kuwa dhamira ya mheshimiwa rais Samia ni njema ya kuhakikisha yale yote yaliyoanzishwa na Hayati Magufuli na yeye akiwa makamu wa rais maana yake walikuwa wanafanya kama timu moja yanakamilika"
"Na kwahiyo yale ambayo yalikuwa hayajaanzishwa lakini ni kero ya wananchi mheshimiwa rais Samia anashughulika nayo...na miongoni mwa hayo ni pamoja na ujenzi wa shule hii ya msingi...kwahiyo niwapongeze sana kwa kupata milioni 400 kujenga shule mpya hii ya kisasa kwaajili ya shule ya msingi" amesema Shigela.
Awali mkuu wa wilaya ya Chato,Deusdedith Katwale,amesema fedha hizo zimetoka serikali kuu na halmashauri imekuwa mstari wa mbele kuzisimamia ili mradi huo uweze kukamilika bila kukwama sehemu yoyote.
Aidha amesema wamekubaliana na halmashauri ya wilaya kuwa na kamati ndogo za usimamizi wa miradi ya ujenzi kutoka serikali za vijiji, lengo likiwa ni kuhakikishaubora wa miradi huku akiwapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuuonyesha katika miradi mbalimbali.
Diwani wa kata ya Kachwamba,Stella Masabile, akizungumza kwa niaba ya wananchi ameelezea changamoto wanazokabiliana nazo licha ya ujenzi huo kufikia aslimia 50 kwa sasa, na kwamba kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi na ubovu wa miundo mbinu ya barabara unaochangia kuchelewesha ujenzi huo kutokana na vifaa kutofika kwa muda mwafaka.
Mwisho.




Post a Comment