DC-MBULU AELEKEZA ASASI ZA KIRAIA KUJIPANGA UPYA.




                                  ************
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, amezielekeza asasi za kiraia wilayani humo Kujitathimini na Kujipanga upya katika Kusimamia Malengo waliojiwekea katika Kusajiliwa Kwake. 

Komred Kheri James ameyasema hayo hii leo katika Kikao Kazi alicho Kifanya kwa Lengo la Kukutana na Kushauriana na Viongozi wa Asasi za Kiraia zinazofanya Shughuli zake Wilayani Mbulu. 

Katika kikao hicho Komred Kheri James amezitaka asasi Kuongeza Nguvu Katika Kupambana na Ukiukwaji wa Maadili,Ukatili na Unyanyasasaji wa Kijinsia,Uharibifu wa Mazingira na Matendo Mengine yote yanayo dumaza Usawa, Haki, Utawala wa Sheria na Ustawi wa watu Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. 

Komred Kheri James ameeleza Kutoridhishwa na Uwepo wa asasi nyingi ambazo hazina Mchango wowote katika kutimiza Malengo ya Kuasisiwa kwake, na hivyo Kawaomba Viongozi wa Asasi Kujitathimini na Kujipanga Upya ili kuisaidia Jamii. 

Kwa Upande wa Mapambano dhidi ya Kuporomoka kwa Maadili, Komred Kheri James amesisitiza Umuhimu wa Kuimarisha Malezi katika Ngazi ya Familia, Shule na Taasisi za Dini ili Kujenga Msingi bora wa Maadili katika Jamii. 

Kupitia kikao hicho, Komred Kheri James amewaahidi Viongozi wa Asasi zote Ushirikiano wa Kutosha na Fursa ya kufanya majukumu yao vyema kwa kadri ya usajili wa kila asasi. 

“Asasi za Kiraia ni Mdau Muhimu Sana katika Maendeleo ya Jamii yetu, Hivyo tutawapa Ushirikiano wa Kutosha ili nia Njema ya Kusajiliwa Kwenu iweze kutimia kwa ufanisi katika wilaya yetu.Na zile asasi ambazo zitafanya Kinyume cha Malengo ya Usajili wake, au Kutumika Kama kichaka cha uovu na uharibifu katika Jamii tutazifuta na kuzichukulia hatua zaidi za kisheria ili liwe funzo kwa wengine,na ili tuweze kuilinda jamii yetu”. 

Viongozi wa asasi za kiraia wilayani Mbulu,wameahidi kuchapa kazi na kuisaidia jamii kupiga hatua za maendeleo kwa kasi zaidi.

0/Post a Comment/Comments