
Baadhi ya waheshimiwa wabunge wakiwasikiliza kwa makini watendaji wa EWURA wakati waliotembelea banda la EWURA leo.
***********
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar.29/05/2023, imetoa elimu ya udhibiti wa huduma za nishati, katika maonesho ya shughuli za sekta ya nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
EWURA imepata fursa ya kuwaelimisha waheshimiwa wabunge kuhusu utaratibu wa kupata leseni za shughuli za umeme, petroli na gesi asilia pamoja na namna ya kujisajili kwenye kanzidata ya watoa huduma na wataalamu kwenye sekta ya petroli na gesi, yaani LSSP.
Post a Comment