GUGU ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO



'                                                                       ''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Serikali Mkoani Dodoma imeendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya Elimu

na Afya kwa lengo la kuboresha na kusogeza huduma kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 02/05/2023 na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma

Bw. Ally Gugu alipofanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Chemba kukagua miradi ya

maendeleo.

Bw. Gugu ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa, maabara na zahanati katika

Vijiji vya Jangalo, Soya na  Ombiri ambapo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho

na umegharimu kiasi cha Shilingi millioni 90.6 kwa madarasa 12 na maabara 1, kwa

upande wa ujenzi wa zahanati umegharimu kiasi cha Shilingi millioni 50.

"Ndugu zangu Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kukamilisha miradi hii ya

maendeleo, nitoe rai kwenu kwanza kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati,

pili miradi ikamilike kwa ubora wa hali ya juu” Gugu amesisitiza.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi. Siwema Jumaa

amesema mbali ya fedha kutoka Serikali kuu utekelezaji wa miradi hiyo ni pamoja na

jitihada za nguvu za wananchi ambao kwa baadhi ya majengo ya zahanati na

madarasa wananchi wamejenga maboma.

Pia, amewataka wakazi wa vijiji vya Jangalo ,Soya na Ombiri kuwa walinzi namba

moja wa miradi hiyo kwa kuwa inaghariimu fedha nyingi za Serikali.

Ziara ya Bw. Gugu ilianzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Chemba na Ofisi ya

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kuongea na watumishi na

kufanikiwa kukagua umaliziaji wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya Msingi

Ombiri, ujenzi wa vyumba tisa vya madarasa, jengo la Utawala, matundu 30 ya vyoo

katika shule ya Msingi Soya, umaliziaji wa chumba 01 cha maabara shule ya

Sekondari Jangaro na ujenzi wa Zahanati ya Mlongia.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu

amefanikiwa kuongea na  watumishi na  kuwaasa  kufanya kazi kwa weledi,

ushirikiano, kupendana na kufanya kazi kwa ubora na kuepuka kufanya kazi kwa

mazoea .

0/Post a Comment/Comments