****************
Na Magrethy Katengu
Wafanyabiashara Kariakoo wa Maduka wamegoma kufungua biashara zao mpaka Mei 19 Ijumaa Mwaka huu Mpaka watakapopatiwa ufumbuzi wa kukutana na Rais w Dkt Samia Suluhu Hassani kuongea nao kuhusu Mgogoro wao na TRA kuhusu ukusanyaji kodi .
Wakizungumza Leo Jijini Dar es salaam katika Mkutano waliokutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla kumweleza namna wanavyokumbana na changamoto na watumishi kutoka Mamlaka ya Mapato TRA Benard Mwakiluwa amesema wamechoshwa na sheria kodi ya stoo mfumo uliopo wa ulipaji kodi kwani ipo tofauti na nchi nyingine hivyo Wateja wao wamewakimbia kutokana na kukamatwa na mizigo yao na huku wengine mizigo yao ikishikiliwa mpaka leo hivyo wanamuomba Rais mwenyewe aje awasikilize kwani siku za nyuma alishaenda Waziri wa fedha, Waziri wa Viwanda na bishara Waziri Mkuu lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya kupewa propaganda huku wao wakiendelea kuumia .
"Kwakweli soko hili wafanyabiashara tumekuwa wazalendo kwa kuvumilia mengi na kila tunapopeleka malalamiko yetu hayafanyiwi kazi hivyo kupitia Mgomo huu tulioamua tufunge maduka yetu mpaka Rais atakapoamua kuja na tukaa naye meza moja kuzungumza na kutusaidia kusuluhisha mgogoro ambao umedumu kwa muda mrefu"amesema Benard
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumiuya wa Shirikisho wa Wafanyabiashara Tanzania Martini Mbwana amesema wamekuwa wakikutana na viongozi mbalimbali lakini wakishatoa maagizo kuzuia operesheni ya watu wa TRA lakini wakishaondoka huku nyuma maagizo yao hayatekelezwi na TRA wanakuja juu na kusema utaratibu uko palepale na kilichoongelewa kinabakia ni siasa hivyo tunaomba jambo hili liangaliwe kwa jicho la tatu na serikali.
Naye Mwenyekiti wa Vituo vyote vya Wafanyabiashara Kariakoo Rwaimamu Erasto amesema inawaumiza sana mlundikano wa Kodi yao mzigo yao kila inapopita wakiagiza kutoka nje ya nchi wanalipishwa kodi wakileta dukani wanalipia kodi bado wanalipia pango bado wanaambiwa kuna sheria ya Kodi ya stoo wakiwauzia wateja nao wanakamatwa kudaiwa kodi kiukweli ni shida hivyo wateja wamewakimbia na kwenda masoko mengine.
Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa Amosi Makala amewaagiza Viongozi wa wafanyabiashara wote kuunda kamati ndogo ambayo itawawakilisha iende Dodoma kukaa meza Moja kuzungumza na Waziri Mkuu na kupeleka kero zao kisha wataletewa ufumbuzi wa jambo hilo lakini Wafanyabiashara hao wamemekubali lakini uamuzi wao ni kuendelea kugoma mpaka watakapokutanishwa na Rais





Post a Comment