HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBITI YAPATIWA MAFUNZO YA UHIFADHI WA MISITU NA UFUGAJI NYUKI

 



                                  """"""""""""
Halmashauri ya wilaya ya Kibiti  mkoani Pwani imeanza kupatiwa  Mafunzo ya Sera ya Misitu na Sera ya Ufugaji Nyuki yakilenga kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wadau wa misitu ili kuwasaidia wakazi wa wilaya hiyo kufanya shughuli za ufugaji nyuki 

Akizungumza leo Mei 4, 2023 wakati akifungua Mafunzo hayo Mtaalamu wa  Nyuki kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Aneth Moshi  amesema  mafunzo  hayo yatawawezesha Wadau hao kutunza misitu ili kufanya shughuli za uhifadhi na ufugaji nyuki kiuchumi.

‘’ Lengo kuu la sisi kuja hapa ni kutoa elimu endelevu kwa wadau wa sekta za misitu na ufugaji nyuki juu sera za Misitu na nyuki,sheria, kanuni na Miongozo mbalimbali  itakayowasadia katika utekelezaji wa majukumu yao na hatimae kufanya sekta hizi kusonga mbele .’’ amesema Moshi.

Naye, Afisa Sheria kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,  Daniel M.Mganga amesema,rasilimali ya misitu na nyuki ni rasilimali ya watanzania wote ambayo imekasimiwa kwa mujibu wa Sheria kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo inabidi itumike kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo  hivyo kupitia mafunzo haya wananchi na wadau muhimu wa sekta ya misitu na nyuki watanufaika kwa kupata uelewa wa Sera na Sheria zinazosimamia sekta hizi muhimu na hivyo kurahisha shughuli za kila siku zinazohusiana na sekta hizi mbili.

"Sheria ya misitu kifungu cha 49 kinaweka masharti ya kuwa na  vibali ikiwemo vya uvunaji, usafirishaji na vingine.Ufahamu wa Sheria zinazosimamia sekta hizi ni suala ambalo wakazi wa eneo hili  wakifahamu itawasaidia kwa kiasi kikubwa."amesema.

Halima Mchinja akizungumza kwa niaba  ya Wanufaika wa  mafunzo hayo  ameishukuru Serikali kwa kuandaa  mafunzo ambayo  yamesaidia kuwapa uelewa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya misitu na nyuki.

0/Post a Comment/Comments